Maalim Seif Anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmin Uzinduzi wa Filam ya Toba Salama Bwawani Kesho.
MAKAMO wa Kwanza wa Rais,Maalim Seif Shariff Hamad, anatarajiwa kuwa mgeni rasmin katika uzinduzi wa filamu ya ‘Toba’ katika ukumbi wa Salama Hall,Bwawani Hotel May 18 mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,Mkuu wa shughuli za uzinduzi huo ambae pia ni muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania,Issa Mussa ‘Cloud’ amesema kuwa filamu hiyo yenye maudhui ya dini ya Kiislamu .
Amesema kuwa katika uzinduzi huo kutasindikizwa Kasida kutoka madrassa mbali mbali za visiwani Unguja huku mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo kupata kuona filamu hiyo.
“Natarajia wageni mbali mbali watakaofika katika uzinduzi huo watafarijika na burudani ambazo tumewaandalia ikiwemo kaswida kutoka katika madrassa mbali mbali,mauled ya homu pamoja na filamu yenyewe,”amesema.
Cloud amefahamisha kuwa filamu hiyo yenye maudhui ya dini ya kiislamu,lengo lake kuwahamasisha waislamu kurejea kwa mola wao na kuachana na vitendo viovu.
Amefahamisha kuwa katika uzinduzi huo pia kutauzwa cd za filamu hiyo pamoja na burudani ya maulid ya homu ya Mtendeni,chuo cha Qadiria Amani na vyuo mbali mbali maarufu visiwani Zanzibar .
Hii ni filamu ya kwanza yenye maudhui ya dini ya kiislamu kuzinduliwa visiwani Zanzibar ambayo imeshirikisha wasanii wengi maarufu wa filamu akiwemo Bi Hindi,Sandra,Cloud na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment