Habari za Punde

Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Karume Jimbo la Rahaleo.


Makamu Mwenyekiti wa  CCM  Zanzibar  Rais Mstaafu wa  Zanzibar  Dk. Amani Abeid Karume, akisalimiana na Wazee wa Jimbo la Rahaleo alipofanya ziara ya kutembelea jimbo hilo kuangalia maendeleo ya Chama katika jimbo hilo, akiwa katika tawi la CCM Muembeladu .
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akipokelewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo, alipokuwa na ziara ya kutembelea Maendeleo ya Chama katika jimbo hilo
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akizungumza na Wanachama wa CCM tawi la Muembeladu alipokuwa na ziara ya Kichama kutembelea jimbo hilo. 
Mwenyekiti wa  tawi la muembeladu  Mshamba akizungumza machache  wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Karume alipotembelea tawi hilo kuona maendeleo ya Chama katika jimbo hilo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Muembeladu wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume akiwahutubia wakati wa ziara yake katika jimbo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume, akiwahutubia Wanachama wa CCM wa Jimbo la Rahaleo katika ukumbi wa Tawi la CCM Gulioni.

 Katibu wa CCM Jimbo la Rahaleo akisoma risala ya jimbo wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume alipofanya ziara kutembelea jimbo hilo.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.