Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji wakati akifafanua jambo wakati alipokuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi, Makazi Maji na Nishati Ramadhan Shaaban katika tafrija ya kuhitimisha Bodi ya usajili wa Wakandarasi iliyofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame akimkabidhi cheti mmoja ya wajumbe wa Bodi ya Kandarasi Zanzibar Said Omar Fakih katika tafrija ya kuhitimisha Bodi hiyo iliyofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini, Picha na Abdulla wa Maelezo Zanzibar
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Imeelezwa kuwa ufahamu wa kazi za Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Zanzibar
umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba mwitikio wa usajili umekuwa ukiongezeka
siku hadi siku.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji wakati alipokuwa
akimuwakilisha Waziri wa Ardhi, Makazi Maji na Nishati Ramadhan Shaaban katika
tafrija ya kuhitimisha Bodi ya usajili wa Wakandarasi iliyofanyika ukumbi wa
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort
Mazizini.
Dk. Mwinyihaji amesema matokeo ya ufahamu
huo yanatokana na kazi kubwa iliyofanywa na bodi hiyo ambayo imemalizika muda
wake na kwamba wajumbe wake bado wanahitajika kutoa ushauri kwa Bodi mpya
ambayo itaundwa tena upya.
“Tunaomba muwe tayari kuwapatia uzoefu wenu
vijana na wajumbe wote ambao watateuliwa katika bodi mpya, bado nyinyi ni watu
muhimu katika nchi hii” Alisema Dk. Mwinyihaji.
Akielezea malengo
makuu ya Bodi hiyo Dk. Mwinyihaji alisema ni pamoja na kusimamia Sekta ya
ujenzi hasa katika ujenzi wenyewe,majirani na hata wapita njia.
Malengo mengine
ni pamoja na kuhakikisha Wakandarasi ambao wanasajiliwa wanapangwa kwenye
madaraja kwa mujibu wa uwezo wao samba na kutoa elimu kwa wakandarasi ili
kukuza uwezo wao.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Ramadhani Kesi aliipongeza Serikali kwa kuwaamini
kusimamia majukumu ya Bodi hiyo ambayo ilikuwa inakabiliwa na changamoto
nyingi.
Miongoni mwa
changamoto ni pamoja na Bodi kuanzishwa kwa muda wote wa miaka mitatu bila
kuwekewa fungu la ruzuku na kuifanya Bodi hiyo kujiendesha yenyewe kwa kusua
sua.
Changamoto
nyingine ni pamoja na kukosa Ofisi na watendaji wa kudumu jambo ambalo limekuwa
likiwakosesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Bodi hiyo
iliyohitimisha kazi zake imeshasajili Wakandarasi katika fani za
majengo,majenzi, umeme na fani maalumu ambapo Wakandarasi 19 kutoka Zanzíbar,10
kutoka Tanzania Bara na Saba kutoka nchi za kigeni wamesajiliwa.
Bodi hiyo ambayo
iliundwa June,2009 inahitimisha kazi zake June 2012 ambapo Waziri wa Ardhi, Makazi
Maji na Nishati Ramadhan Shaaban anajukumu la kuunda Bodi mpya ili kuendeleza
majukumu yaliyoachwa na Boda hiyo.
IMETOLEWA NA
HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:
Post a Comment