Habari za Punde

Mbunge wa Kikwajuni Afanya Ziara Atembelea Miradi ya Maendeleo ya Jimbo hilo.b

 
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni(kulia) akimkabidhi Sheha wa Kilimani Halid Ali, makabidhiano hayo yamefanyika Kilimani Juu. 
 Mbunge Hamad Yussuf Masauni na Diwani wa Kilimani na Wananchi wakiwa katika zoezi la uchimbaji waa usambazaji wa mipira ya maji kwa wananchi wa kilimani
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi mipira ya maji na Tangi la kuhifadhia maji yanayotoka katika kisima na kusambaza kwa wananchi wa shehia hiyo.
 Wananchi wa Kilimani wakichimba mitaro ya kuweka mipira ya kusambaza maji katika majumba ya kilimani kuunganisha na kisima kilichochimbwa na Mbunge.
 Mwananchi wa Shehia ya Kilimani Seif Omar, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la uchimba mtaro kwa ajili ya kuweka mipira ya maji, ili kusambaza maji safi na salama katika majumba ya kilimani baada ya kukabidhiwa na Mbunge wao,kuunganisha kisima kilichochimbwa kilimani juu ili kutowa huduma kwa Wananchi wa Kilimani. 
 Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni, akiwa na Viongozi wa jimbo hilo wakikaguwa ujenzi wa barabara ya hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya jimbo hilo.
 Mdau mambo ya ujenzi wa barabara ya ndani jimbo la Kikwajuni ikiwa tayari imewekwa kifusi ikiendelea na ujenzi wake.
Mbuge wa Jimbo la Kikuwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na waandishi na wananchi alipofanya ziara ya kutembelea jimbo hilo na kuangalia miradi ya maendeleo na kukagua ujenzi wa barabara ya jimbo hilo inayotengenezwa kwa kiwango cha lami, kutoka Kikwajuni kwa Kamanda hadi kuungana na barabara ya michezani mao.
Naibu Sheha wa Kikwajuni Juu Jaha Ame Rajab. akizungumza na waandishi wa habari juhusu maendeleo ya ujenzi wa bnaraba hii ya Kikwajuni Mao, wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo hilo kutembelea miradi ya jimbo hilo.

1 comment:

  1. Siku moja nilipokua naangalia mtandao wa bunge niligundua Massauni ni miongoni mwa wabunge wachache wa Z'bar waliosoma vizuri.

    Lkn. kama ilivyo kawaida ya Wazenji wengi makeke yake bado hayajaonekana vizuri. tulitarajia ajitokeze sana ktk BLOG mbalimbali za Z'bar na kutoa ufafanuzi wa mambo mbali mbali kama vile wenzake akina ZITTO, NAPE, TUNDU LISSU N.K

    Sijui tena na hii bara bara ya mtaa itakua na mitaro au ndio yale yale?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.