Habari za Punde

Mjasiriamali wa Kisiwani Kwa Bint Abeid Pemba.

 Mjasiriamali wa Kisiwani kwa Binti Abeid Pemba Riziki Mussa, akionesha bidhaa zake anazozalisha katika sha,ba lake la ufugaji wa ngombe wa maziwa kwa kushirikiana na Vijana aliowaajiri kwa ajili ya kushindika maziwa na kuzalisha siadi na samli. kutokana na malighafi ya Maziwa ya Ngombe, amesema shughuli hiyo inamuigizia kipato na kutowa ajira kwa Vijana wa sehemu hiyo kufanya shughuli za ufugaji na ukamuaji wa maziwa ili kuzalisha Bidhaa hizo.

 Matunda ya Kisiwani kwa Binti Abeid. Samli ya Pemba hiyo mdau  

3 comments:

  1. Hongera wana Kaole. Mwanzo ni mgumu lakini inshaallah utaendelea umfikie blue band na zaidi

    ReplyDelete
  2. Hapa serikali lazima itie mkono wake kwa kuwaelimisha zaidi watu kama hawa na kiwapa motisha zaidi.Hii bidhaa ipatiwe kwa kuanzia soko la ndani (Zanzibar) , na utaalam ukizidi basi soko la nje pia.Huyu inabidi apunguziwe kodi ili aweze kuhimili ushindani wa biashara(hata ulaya ndo zao siku hizi) au apewe unafuu katika usafirishaji wa bidhaa yake ,aikiitoa hapo alipo kwa kuipeleka Chake,Wete,Mkoani au hata Unguja.
    Mwananchi akianzisha kitu serikali lazima imsaidie ili tupeane ajira bila ya kuitegemea serikali.
    Hongera wewe na wengine wenye vikundi kama vyako.

    ReplyDelete
  3. HONGERA MKUU KWA JITIHADA YAKO MUNGU AKUZIDISHIE NA KAMPUNI YAKO IZIDI KUENDELEA KUWA KUBWA NA KUPATA SOKO HATA NCHI ZA NJE INSHALLAH

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.