TIMU ya soka ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa nchi zisizo wanachama wa FIFA, VIVA World Cup, baada ya kuifunga Tamil Elaam mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B, uliofanyika usiku wa jana mjini Erbil, Kurdistan.
Katika mchezo huo, mabao ya Zanzibar Heroes yalitiwa kimiani na Hamisi Mcha dakika ya 22, Amir Hamad dakika ya 61 na Awadh Juma dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, Zanzibar itacheza na Cyprus katika Nusu Fainali kesho saa 3:00 usiku Uwanja wa Suleimaniya, nje kidogo ya mji wa Erbil
Wachezaji wa Zanzibar Heroes Wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbuBendera ya Taifa la Zanzibar ikituwakilisha wakati wa wimbo wa Taifa
Timu zikisikiliza nyumbo za taifa za nchi mbili
Captain Nadir Haroub Cannavaro akiwa katika picha ya pamoja na Marefa na captain wa Timu ya Tamil
Heka heka katika lango la Zanzibar Heroes hata hivyo haikuleta athari yoyote
No comments:
Post a Comment