Ukimuangalia vizuri zaid ni mama ambaye tayari amekwishachoka ima anatoka Shamba au kununua Makozi ya kumtosheleza kupikia kwa siku kadhaa akifika nyumbani kupika kunamsubiri
Huu ni ujumbe unaosomeka katika moja ya daladala na 510 ikisiburi wasafiri stendi kuu ya Daladala Darajani
Mfanyakazi wa Baraza la Manispaa akiwajibika katika kuweka safi mazingira ya Manispaa ya mji wa Zanzibar. Wawakilishi wametoa wazo kwamba huduma hii ibinafsishwe au itolewe tenda kwa watu wengine na baraza kuelekeza nguvu zaidi katika kukusanya mapato
Bi Kidude binti Baraka mwimbaji mkongwe wa visiwa hivi na celebrity wetu alipokutwa mitaa ya Michenzani akifurahiwa na vijana wanaotaka kujua siri ya mafanikio yake.
Pole Mama zangu; aliyebeba kuni na anaetembeza baro la taka, serikali iwaonee huruma mama zetu hawa katika karne hii iliyojaa utaalamu ni haki kweli kuwaadhiri Mama zetu hawa?
ReplyDeleteMasikini Mama zetu.
Mimi nampa hongera Bi kidude kwa kuanza kuvaa viatu!
ReplyDeleteHuyo mama unaemsikitikia analipwa mshahara na hiyo ni kazi kama zilivyo nyengine zile zama za wanawake kukaa ndani zimekwisha...wakija wamama wa kibongo hapo muanze kelele!
Na huyo mwenye kuni kwa alivyo vaa anaonekana ameshuka gari kutoka shamba kwao kaamua kuchukua zawadi ya makozi kwa vile anaishi mjini, wakusaidiwa na serikali sio hawa!
Nitashangaa sana adhubany ukiniambia kwamba angelikuwa ni mama,mke ama jamaa yako usingeliwaonea imani wanawake hao, hao hao wasubiriwe nyumbani kwa kazi nyengine pia! Je, Serikali itapoekeza katika utaalamu wa nishati ya gesi,jua na upepo kutengeneza umeme mwanamke wa mwanzo aliebeba makozi asingepungukiwa na adha hii kwa kuwa na jiko lake litalomsaidia?
ReplyDeleteNa Je mwanamke aliebeba bero ungelihisije kama angelikua ana kijigari cha kuchukulia taka hizo badala ya kutumia nguvu zake (si masihara kuburura bero kwa mwanamke - mwanamme analikimbia hilo); na nyumbani pia kazi zinamsubiri!
Nani kasema kwamba wanawake hawaruhusiwi kufanya kazi? bali ni kazi hizo za ubavu bila kujengewa mazingira ya kufanya kazi kwa urahisi?
Naona umekuwa mtaalamu wa kusoma picha; ulijuaje huyo mwanamke alie na makozi kashuka gari kutoka kwao na hayo makozi ni zawadi!? Na mshahara anaolipwa msukuma bero unakidhi kuutetea utumikaji wa mwanamke kwa kazi kama hiyo, seuze mwanamme?
Na ungelitufahamisha katika jamii wa kusaidiwa mwanzo ni nani tukafaidika.
Ah..haya!..nakubali matokeo, lakini huyu mama wa kwanza kwa alivyo vaa anatokea shamba tena sijui kama si Ndijani!
ReplyDelete