Habari za Punde

Abambwa na Zaidi ya Kilo 14 za Bangi


Na Masanja Mabula, PEMBA
JESHI la polisi mkoa wa Kaskazini Pemba limefanikiwa kumkata mtu anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara maarufu wa bangi, Hamad Hamad Bakari (70) mkaazi wa Jitenge shehia ya Mchangamdogo wilaya ya Wete.

Taarifa za jeshi hilo zimeeleza kuwa wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiahsra huyo wa bangi akiwa na mafurushi 74 yenye uzito wa zaidi ya kilo 14.


Mtuhumiwa huyo ambaye ni mlemavu alikamatwa jana majira ya saa 4:30, asubuhi kufautia taarifa zilizotolewa na raia wema kwa jeshi la polisi ambalo liliweka mtego uliofanikisha kumkata mfanyabiashara huyo.

Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamaishna Msaidizi Mwandaamizi Yahya Rashid Bugi, alisema alisema baada ya raia wema kutoa taarifa jeshi la polisi kwa kushirikiana na polisi jamii liliweka ulinzi na kufanikiwa kukamata majani hayo yakiwa kwenye mapolo.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa wananchi ambao walidai kuchoshwa na tabia ya mtuhumiwa ya kuendelea kuuza bangi, na alipokamatwa alikiri kuwa bangi hiyo ni mali yake na iliingia kisiwani hapa ikitokea Tanga kupitia bandaari ya mtambwe”,alisema Bugi.

Alisema kuwa baada ya kukiri kuwa hiyo bangi ni mali yake, mtuhumiwa aliomba msamaha akiahidi kutorejea tena kosa kama hilo, jambo ambalo kamanda Bugi alipingana nalo na kwamba anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

Kutokana na kitendo hicho, Kamanda Bugi aliwataka wananchi hasa wanaoishi karibu na bandari kutoa ushirikiano na jeshi la polisi kuwafichua wanaoingiza dawa za kulevya ili kuwakinga vijana na wimbi la utumiaji wa dawa hizo.

Alisema wananchi wa Jitenge Mchangamdogo wamechoshwa na vitendo hivyo na kuamua kuondoa muhali na kumfichua mfanyabiashara huyo.

"Lazima tuonde muhali tuwe tayari kuwahoji wananchi wanaopita katika sehemeu zetu wakiwa na mizigo ambayo tuna itilia mashaka, ambapo kwa kufanya hivyo tutaweza kudhibiti uingiazji na uuzaji wa dawa za kulevya hpa nchini", Bugi.

Hata hivyo taarifa zilipatikana na Zanzibar Leo zinasema kuwa mtuhumiwa aliwahi kukamatwa akiwa na majani makavu yanasadikiwa kuwa ni bangi miaka kadhaa iliyopita ambapo aliahidi kutorejea biashara hiyo baada ya kupelekwa mahakamani.

Aidha baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi walivitaka vyombo vinavyosimamia sheria kukunjuka na kutoa adhabu kali kwa wanaokamatwa na dawa za kulevya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.