Habari za Punde

Zaidi ya bilioni 15 Zasamehewa Kodi


Na Husna Mohammed
SHILINGI bilioni 15.794 zimesamehewa kodi na Serikali katika taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizokuwa za kiserikali katika kipindi cha Julai 2011 hadi Aprili mwaka huu.

Taasisi zilizosamehewa kodi ni pamoja na wawekezaji, taasisi za Seikali, kampuni na watu binafsi , miradi ya washirika wa maendeleo, mashirika ya Umma na taasisi za kidini.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee, aliliambia baraza la wawakilishi jana wakati akijibu suala la Ismail Jussa Ladhu, Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, aliyetaka kujua misamaha mingapi ya kodi na ushuru, thamani yake na nani walionufaika, sambama na  kulingana na kutofautiana  vipi.

Waziri Yussuf, alisema katika kipindi cha Julai hadi Juni 2010/2011 jumla ya shilingi bilioni 18.389 sawa na asilimia 100 zilikuwa ni misamaha kwa taasisi hizo.

Hata hivyo, waziri huyo alisema kuwa msamaha huo umekuja kutokana na mamlaka iliyopewa uwezo wa kutoa misamaha hiyo ambayo ni wizara inayoshughulikia fedha.

Aidha alisema Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), ina jukumu la kukusanya na kuratibu maombi ya misamaha (ZRB) ambapo kamati hupokea, huzingatia ma baadae kumshauri Waziri anaeshughulikia Fedha kwa maingatiao na uamuzi wa kutoa misamaha hiyo.

3 comments:

  1. SMZ kumbe hawako "serious" yaani sehemu yenye uchumi mdogo kama Z'bar unasamehe kodi bilioni 15?..Kumbe ndio maana serikali inashindwa kutoa huduma za jamii kikamilifu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bilioni 18 ni asilimia ngapi ya mapato yaliyokusanywa na yale yaliyoweza kukusanywa? Ni vema tungepewa na MCHANGANUO wa aina za kodi na ushuru ulosamehewa na kiashi chake husika.

      Delete
  2. Kuna ugumu gani kwa wizara ya fedha, KILA MWEZI kuchapisha orodha ya wale wote waliofaidika na misamaha hiyo ili wananchi sote tupate taarifa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.