Joseph Ngilisho, ARUSHA
ABILIA zaidi ya 3,000 wanaosafiri kati ya Arusha na
Moshi wameshindwa kupata huduma hiyo kwa wakati baada ya gari basi aina
ya Coaster zinazosafirisha abiria katika mikoa hiyo kugoma.
Kwa mujibu wa wamiliki wa gari hizo wanapinga ongezeko la ushuru katika kituo cha mabasi cha Moshi kutoka shilingi 1,000 hadi shilingi 2,000 kiasi ambazo wamedai hawataweza kukilipa.
Hali hiyo imesababisha wengi wao kushindwa kufika kwa wakati huku baadhi ya abiria wakisota kwa muda mrefu kituoni wakisubiri usafiri huku wengine wakifanikiwa kudandia gari ziendazo Dar es Salaam, Tanga na Morogoro na kutozwa nauli kubwa tofauti na ile iliyozoeleka ya shilingi 2,500.
Baadhi ya wamiliki wa gari hayo, Emanuel Kisamo na Yohani Muro walisema kuwa ongezeko la shilingi elfu moja na kufikia shilingi 2000, kwao ni kubwa na hawatawezi kumudu kulipa kiasi hicho.
Walidai kuwa walijumulisha malipo yote ya ushuru wanayotozwa njiani inafikia kiasi chga shilingi 8000 kwa safari moja,hali ambayo wamedai ni hasara kwao na itawafanya waachene na biashara hiyo.
Aidha wameiomba halmashauri ya mji wa Moshi kuondoa ongezeko la shilingi 2,000 na kuacha tozo la zamani la shilingi 1,000 kama ambavyo wanatozwa katika kituo cha mabasi cha Arusha.
No comments:
Post a Comment