Na Mwantanga Ame
SERIKALI ya Zanzibar imetenga shilingi milioni 140 kwa ajili ya shughuli za kuhifadhi mazingira katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedfa, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee aliyasema hayo jana wakati akizungmza na Zanzibar Leo huko Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri Omar alisema serikali imeamua kuweka kiasi hicho cha fedha ikuwa ni hatua ya kuimarisha mkakati wa kupambana na athari za kimazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema fedha hizo zimetengwa baada ya kujitokeza tatizo kubwa la watu kutopenda kutunza mazingira kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uharibifu jambo ambalo tayari baadhi ya maeneo yameonesha kuwapo kwa athari hizo.
Aidha, alisema zoezi hilo serikali italifanya kwa kushirikia ana watendaji katika taasisi nyengine ikiwemo Idara kuu ya kusimamia mazingira, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Wanafunzi wa skuli na watendaji mbali mbali kutoka katika taasisi zaa serikali.
Akitaja sababu kubwa ya kufanyika zoezi hili Waziri huyo alisema hapo awali serikali ilishindwa kuweka bajeti halisi kwa ajili ya kuhudumia eneo la mazingira lakini kutokana na umuhimu na ahadi ya Rais kuhakikisha analinda mazingira wameamua kuanza hivi sasa.
Alisema mazingira ya Zanzibar bado hayako katika hali nzuri kutokana na baadhi ya watu kuamua kutumia vibaya raslimali za nchi katika kutunza mazingira.
Alisema kutengwa kwa fedha hizo zitawezesha kutumika ili kuhakikisha hali ya mazingira Zanzibar, inabakia kama ilivyo ili kuweza kusaidia kupunguza kutokea athari zaidi.
No comments:
Post a Comment