Habari za Punde

Pongezi kwa Dk Shein kutoka Canada


Kwa niaba ya wana-Diaspora wote nchini Canada, Kamati Tendaji ya Zanzibar – Canadian Diaspora Association (ZACADIA) inachukuwa fursa hii kutoa salamu za hongera kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kwa agizo alilolitoa la kununuliwa meli kubwa mpya ya abiria wapatao 1000 na yenye uwezo wa kuchukua mizigo ya tani 100 ambayo itawaondoshea shida na usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri kati ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.