Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Awasili Zanzibar akitokea Ziara Maalum Nchini Uingereza.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(wa pili kulia) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, na Viongozi mbali mbali wa vyama siasa Serikali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati alipokuwa akirejea Nchini,akitokea nchini Uimgereza kwa ziara
maalum,katika safari hiyo alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pampja na Maofisa wa serikali.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati alipokuwa akirejea Nchini,akitokea nchini Uimgereza kwa ziara maalum,katika safari hiyo alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pampja na Maofisa wa Serikali.(Picha na Ramadhin Othman)

2 comments:

  1. Kuwepo kwa Pinda katika mapokezi ya Dk. Shein, ni ishara mbaya sana. Kunanipa wasiwasi sana na lazima, tena nasisitiza kuna jambo hapo. Hata nyuso za Pinda na Balozi Seif zinazungumza ajenda chafu imejificha mioyoni mwao.
    Sasa, naanza kupata mashaka na ziara ya Dk Shein na Kikwete, London.
    Nikichanganya na picha aliyoionesha Jussa baraza la wawakilishi, ikimuonesha Kikwete akitia saini mambo yahusuyo uchimbaji wa mafuta Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Tuacheni uoga usio na msingi, kwanini tumshangae Pinda kuwepo Z'bar na yeye ni waziri mkuu wa TZA ambayo Z'bar ni sehemu?

    Kimsingi hayupo Z'bar kumpokea Dr. Shein bali imesadif yeye kurudi ziarani na waziri mkuu yupo visiwani.

    Sasa tukianza kusoma sura za watu na kjifanya tuna 'ilmul ghaib' tutakua tunakosea.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.