TAARIFA KWA BARAZA LA WAWAKILISHI JUU YA USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ KUPITIA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI ZANZIBAR MARITIME AUTHORITY – ZMA
Mhe. Spika,
Tarehe 27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania (The Citizen) na nchi za nje (International news Agency – Bloomberg) viliandika makala kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN.
Gazeti la “The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012 lilikuwa na kichwa cha habari “Iran Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo” (meli za mafuta za Iran zinatumia bendera ya Tz kukwepa vikwazo.
TAARIFA YA ZMA
Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).
Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:
Section 8 (1). There shall be established the registers of Tanzania Zanzibar ships to be Known as:-
(a). Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean going ships; and
(b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.
(2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of this Act if that ship is registered under this part.
Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. (Open Registry).
Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.
Kama nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari vimechapisha makala ya usajili wa meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN kulingana na makala zao hizo.
SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:
Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka
1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta
2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus
3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta
4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta
5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus
6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta
7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta
8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta
9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus
10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus
11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus
Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons
Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration).
Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda usajili wa “TUVALU Islands”.
ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya IRAN.
Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli
ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry).
Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine (PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na Malta.
Kinyume na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari juu ya uraia wa wamiliki wa meli hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza katika usajili wa meli zao wana uraia wa British Vergin Islands na Sychelles.
Kulingana na “United Nations Convention Law of the Sea”, Article 91, na za “Geneva convection of Registration” articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar Maritime Transport Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa zinazoongoza usajili huo.
Maelezo haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi kuwa Zanzibar imesajili meli za IRAN ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya (European Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta kutoka Iran.
Mhe. Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yeyote zaidi ya kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka kusajili meli zao kwetu.
Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi.
Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi wake.
Hata hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa kitaifa na kimataifa katika biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli zinasajiliwa chini ya mamlaka hii zinafata taratibu ilizoweka.
Mhe. Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya habari (The Citizen), Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe) alipokuwa akijibu suala Bungeni hivi juzi hakuonyesha kurishiki kwake katika usajili wa meli (Open Registry) inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara ya kuja Zanzibar kuonana na Waziri anaehusika kuzungumzia suala hili.
Taarifa za “The Citizen” zaweza kuwa ni muendelezo wa Mhe. Mwakyembe kutoridhika kwake katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia uwakala wake huko Dubai.
Mhe. Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yeyote.
Hili ni suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali yetu ni njia moja ya kuongeza mapato yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili huo hauvunji sheria za Kimataifa.
Mhe. Spika,
Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo.
Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu.
Hivyo, kwa taarifa hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo vya habari kuhusiana na suala hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo juu.
Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.
Hamad Masoud Hamad
WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
ASANTE MH WAZIRI TUMEKUFAHAMU VIZURI NA UZI HUO HUO,HIZO NI FITNA ZA HAO WASIO ITAKIA MEMA ZANZIBAR YETU WAKIONA SISI TUTAPATA TONGE TUWEKE MDOMONI WAO WANAANZA HABARI ZAO ZA KIPUMBAVU NA UZUSHI.NDO MAANA TUMECHOKA TUNATKA TUACHWE TUPUMUWEEEEEEEE.
ReplyDeleteHamna lolote, hii kauli inatoka kwa sababu mabwana zenu hawajafika Zanzibar, ila naamini mara tu Mwakyembe akikanyaga Zanzibar mnaweza kubadlilisha hata hili tamko. Zanzibar itaendelea kupoteza fursa anuai za kukuza uchumi wake maadamu inaendelea kuung'ang'ania muungano ambao umewazunguka na kutoruhusu hata kuweza kukuza kipato chake kwa kiwango kidogo. Viongozi wa SMZ kuna mengi ya kujifunza kupitia suala hili, moja wapo ni namna upande wa pili usivyoitakia mema Zanzibar. Pole zenu!
ReplyDeleteNadhani hii ni tamaa mbaya ambayo Serikali ya Zanzibar imekwaa kisiki. Meli zimekuja kusajiliwa Zanzibar ili kukwepa vikwazo vya serikali ya Marekani. Sasa hii imekaaje. Zanzibar haiwezi kuwa na ubavu wa kupigana ma marekani. Ingekuwa hizi ni meli za kawaida ambazo zimevutiwa na gharama tu, basi ingekuwa sawa, lakini hawa ni sawa na wahalifu wanaotafuta pa kujifichia. Hili haliwezekani. Meli za aina hii hazistahiki kupepea bendera ya Tanzania.
ReplyDeleteWashenzi na wapumbavu wakubwa!! Zanzibar ni taifa kamili kama ilivyo kwMarekani hivyo ina haki ya kujiamulia mambo yake bila ya kuingiliwa na taifa jingine liwe kubwa au dogo provided kwamba uammuzi huo hawendi kinyume na sheria na taratibu za kimataifa.
ReplyDelete