Habari za Punde

Balozi Seif afungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Jimbo la Kitope

 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Kaskazini B wakijiandaa kwaUchaguzi wa Viongozi wao watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Uchaguzi huo umefanyikakatika Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini B.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya ccm Balozi Seif Ali Iddi akiufunguaMkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Wil;aya ya Kaskazini Buliofanyika katika Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Wilaya yaKaskazini B.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya Wazazi Wilaya ya Kaskazini B Balozi Seif Ali Iddi akipiga kura kuchagua Viongozi watakaoiongoza Jumuiya hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo hapo kinduni Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope.

NA Othman Khamis Ame

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halamshauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi  Balozi Seif Ali Iddi alisema uwezo na uhakika wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM utaendelea kupatikana iwapo Viongozi wake watakuwa makini katika ubunifu wa mbinu za kuiendesha Jumuiya hiyo.
 
Balozi Seif alieleza hayo wakati akiufungua MkutanoMkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kaskazini “B” uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope iliyopo KinduniWilaya ya Kaskazini “B”.

Balozi Seif ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema umakini wa Viongozi hao hupatikana baada ya Wananchama wenyewe kutoa maamuzi sahihi katika kuwachagua Viongozi wenye sifa hizo.
 
Aliwatahadharisha Wanachama  hao kuwa wakikosea katika  mchakato huo wa uchaguzi wa Viongozi bora ambao hueleweka kutokana na Historia yao waelewe kwamba wamepata hasara katika kipindi chote cha miaka mitano ijayo.
 
“ Tunataka Viongozi wabunifu ambao watakuwa na uwezo kamili wa kuiendelea Jumuiya Kiuchumi sambamba na uimarishaji wa Chama kwani sivyema kujibweteka kwa kutegemea ruzuku kutoka ngazi za juu”. Alisisitiza Balozi Seif.
 
Aidha alieleza kwamba Jumuiya hiyo inakokwenda ni kugumu sana, hivyo nguvu za Chama inazitegemea Jumuiya zake katika kupanga safu bora ya kuendeleza ushindi wa Chama hicho katika chaguzi za miaka mingi ijayo.
 
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifaya CCM aliupongeza Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kaskazini B kwa kusimamia vyema chaguzi za Matawi na Majimbo ndani ya Wilaya hiyo.
 
Aliwataka Viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza Jumuiya hiyo katika misingi ya Uadilifu na Hekima ili lile lengo la kuanzishwakwa Jumuiya hiyo likiwemo la malezi liweze kufikiwa ipasavyo.
 
Akizungumzia suala la Malezi ya Vijana na Watotoambalo limo ndani ya dhamana ya Jumuiya hiyo Balozi Seif alikumbusha kwambaViongozi hao wana kazi ya ziada ya kuliokoa kundi kubwa la Vijana linaloonekanakutumbukia katika wimbi la maovu.
 
Balozi Seif alifahamisha kuwa Vijana wengi Mitaanihivi sasa wameharibika na ni lazima kwa Viongozi hao kusimia ipasavyo katikakuwarejesha kwenye maadili sahihi.
 
“ Heshima ya Watoto wetu siku hizi iko katika kiwango cha chini ikilinganisha na enzi za utoto wetu sisi. Hii ni hatari na balaa iliyotuzunguuka. Tusitarajie Mtu au Taasisi ya Nje ya Nchi kuja kuturekebishia hali hii”. Alitahadharisha Balozi Seif.
 
Alishauri kuongezwa kwa Skuli za Jumuiya katika njia ya kujaribu kurejesha maadili Nchini kwani hili ni Jukumu lao katika kuielimishaJamii.
 
“ Inasikitisha kuona Jumuiya hiyo ina Skuli chache tu hapa Nchini wakati suala la kuielimisha Jamii limo ndani ya dhamana yao”. Aliongeza Balozi Seif.
 
Mapema akitoa Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya hiyo katika kipindi kilichopita Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya yaKaskazini “B” bibi Mwanaidi Salum Kidemea alisema Jumuiya yao bado inakabiliwa na changamoto kadhaazikiwemo uhaba wa Vifaa vya Kazi.
 
Bibi Mwanaidi alisema katika kipindi kijacho Jumuiya hiyo imelenga kuongeza wanachama zaidi kwa nia ya kupata nguvu za kujiandaa naushindi katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.
 
Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kaskazini B tayariimeshapata Viongozi   katika ngazi zaMatawi na Majimbo yote ya Wilaya hiyo baada ya kukamilisha zoezi la uchaguzi kwenyengazi hizo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.