Karani wa Sensa Asha Iddi Aslan, akijaza dodoso wakati akimuhoji Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif SharifHamad, huko nyumbani kwake Mbwezi, Zanzibar.Picha na Salmin Said OMKR
Na Hassan Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad leo amekuwa miongoni mwa viongozi nawananchi walianza kuhesabiwa katika zoezi linaloendelea la sensa ya watu namakaazi.
Makarani wa sensa wakiongozwa na msimamizi wa makarani bibi Asha Iddi Aslan walifika nyumbani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mbweni mnamo majira ya saa nne asubuhi kwa ajili yakuwasilisha dodoso la sensa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Sharif Hamad amesema zoezi hilo limeenda vizuri, na kuwataka makarani wa sensa kuendelea kuwa waadilifu na wavulivu katika kufanikisha kazi hiyo.
Amesema inawezekana kuwa baadhi ya watu hawakupata elimu ya kutosha kuhusu sensa, lakini kwa wale walioelimishwa na kuendelea na msimamo wao wa kukataa kuhesabiwa huenda wakawa na malengo yao binafsi.
“Wanaokataa kuhesabiwa inawezekana wana malengo yao ambayo hawajataka kuyaweka wazi”, alisema MaalimSeif.
Amesema msimamo wa Serikali pamoja na Chama chake cha CUF ni kutaka watu wote wahesabiwe katika zoezi hili linaloendelea, ili kuisaidia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo.
Amefahamisha kuwa zoezila sensa ni jambo la kawaida katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo nchi zakiislam, na kutoa wito kwa wananchi kutokubali kuyumbishwa na badala yakewaitikie wito wa Serikali wa kukubali kuhesabiwa kwa maslahi yao na taifa kwajumla.
No comments:
Post a Comment