Habari za Punde

Rais Kikwete, Dk Bilal wahesabiwa katika sensa ya watu na makaazi leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete na familia yake  akijibu maswali toka kwa karani wa sensa ya watu na makaazi Bw. Clement Ngalaba leo Agosti 26, 2012
wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima.


PICHA NA IKULU

MAKAMU waRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makaziakiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bilal,ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karaniwa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamuakiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutokaOfisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.

Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37,yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.

Akizungumzabaada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwaujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo,ambalo litadumu kwa siku saba.

                                               Imetolewana Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.