Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akisalimiana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba katika chakula cha Futari aliyowaandalia wananchi na waumini Kijiji cha Mkanyageni katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akijumuika na wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba,katika chakula cha Futari,aliyowaandalia Wananchi hao katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni jana
Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba jana
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,(katikati) akijumuika na akinamamawa wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba katika Chakula cha Futari iliyoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni wilaya ya Mkoani Pemba jan
Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba jana
Sheikh Yussuf Abdalla,wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba akitoa shukurani kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Moahmed Shein,kwa kuwaandalia Chakula cha Futari,iliyofanyika jana katika Viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiagana na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba jana baada ya Chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni. {Pichana Ramadhan Othman,Ikulu.}
Na Rajab Mkasaba, Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein jana aliungana na wananchi wa Mkanyageni Chokocho katika futari maalum aliyowatayarishia wananchi hao huko.
Hafla hiyo ilifanyika huko katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba na kuhudhuriwa na wananchi mbali mbali wa maeneo hayo na jirani pamoja na viongozi wa dini, Serikali na vyama vya siasa.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba Mhe. Jabu Khamis Mbwana, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Mwinyihaji Makame, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih na viongozi wengine.
Akitoa neno la shukurani kwa wananchi waliohudhuria futari hiyo kwa niaba ya Rais Dk. Shein, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Jabu Khamis Mbwana alisema kuwa Dk. Shein amefarajika kwa ushiriki wa wananchi hao katika futari hiyo maalum aliyowaandalia na anawatakia kila la kheri.
Mhe. Jabu aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kuendeleza upendo miongoni mwao kwa maslahi yao na maslahi ya nchi kwa ujumla.
Alieleza kuwa mbali ya shukurani hizo pia kuna haja ya kukumbushana mambo ambayo yanaendelea nchini ikiwa ni pamoja na mchakato wa marekebisho ya Katiba na kuwataka wananchi washiriki kikamilifu kutoa maoni yao sanjari na kushiriki siku ya Sensa inayotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
Nae Sheikh Abdalla Yussuf, akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wananchi hao alieleza kuwa utamaduni huo aliojijengea Dk. Shein wa kuwafutarisha wananchi hao ni jambo la msingi na lina manufaa makubwa sana kwao na hata mbele ya MwenyeziMungu.
Katika neno lake hilo la shukurani Sheikh Yussuf alieleza wananchi wa maene hayo wamefarajika na uongozi wa Dk. Shein na wanatambua juhudi kubwa anazozichukua katika uongozi wake kwani amekuwa akifanya kazi usiku na mchana kwa maslahi ya nchi na wananchi wake.
Pamoja na hayo, wananchi hao walipongeza juhudi za kuendeleza amani na utulivu uliopo nchini ambao umepelekea kuwepo kwa maendeleo makubwa.
Akielezea juu ya umuhimu wa sense kwa wananchi wa Zanzbar, Sheikh Yussuf alisema kuwa anawashangaa wale wote wenye mtazamo hasi juu ya zoezi hilo na kusisitiza kuwa inaonesha wazi wanapingana na kitabu kitukufu cha MwenyeziMungu yaani Qur-an,
Kutokaa na hilo, Sheikh Yussuf alieleza kuwa ipo haja kwa waumoni hasa wa din ya Kiislamu kuisoma sana Qur-an ili waweze kujua umuhimu wa hesabu ulivyoweka katika kitabu hicho kitukufu.
Alisema kuwa maisha yote ya binaadamu yamewekwa kwa hesabu na kueleza kuwa zoezi la sensa husaidia katika upangaji, utafiti na tathmini ambayo yote hayo ni muhimu sana kwa mwanaadamu.
Wananachi hao walimuombea dua kwa MwenyeziMungu na kumuombea aendelee kongoza nchi kwa salama, amani, utulivu na uvumilivu mkubwa pamoja na kupata maendeleo endelevu nchini.
Katika futari hiyo, Mama Mwanamwema Shein nae alishiriki akiungana na akina mama wenzake kutoka sehemu mbali mbali za maeneo hayo pamoja na viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa na wananci kwa ujumla.
Dk. Shein na mama Mwanamwema Shein pamja na ujumbe aliofuatana nao wamereja Unguja leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment