Habari za Punde

Jaji Bomani akutana na tume ya mabadiliko ya katiba


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba (kulia) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wajumbe wa Tume kabla ya kumkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu Jaji Mark Bomani (kushoto) kubadilishana uzoefu na Wajumbe wa Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumamosi, Agosti 3, 2012). Wengine ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid na Naibu Katibu Bw. Casmir Kyuki (kulia)

Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Kwanza Mzalendo Jaji Mark Bomani akibadilishana uzoefu na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumamosi, Agosti 3, 2012). Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim.

Baadhi ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakifuatilia maelezo ya Jaji Mark Bomani aliyekutana nao kwa lengo la kubalishana uzoefu kuhusu Katiba. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumamosi, Agosti 3, 2012)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.