Habari za Punde

Balozi Seif ziarani Bweleo

 Mmiliki wa eneo la Magofu ya Bwefum Bwana Chandra akitoa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhusiana na eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wananchi wa Kijiji Hicho. Balozi Seif alizitaka pande hizo kuwa na subra na Serikali kuu inafanya utafiti utakaopeleke maamuzi sahihi ya mgogoro.
 Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa Uwanja unatarajiwa kuwa wa Kimataifa wa Bweleo Bwana Hassan Gharib akimpatia ufafanuzi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhusiana na changamoto wanazoipambana nazo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Ushirika cha Ukweli ni njia safi wa Kijiji cha Bweleo iliyomshawishi kununua baadhi ya bidhaa hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alio Iddi akiangalia majengo ya skuli ya Bwefum ambayo Mapaa yake yako katika hali mbaya. Kulia yake ni Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo bwana Kesi Mwinyi Shomari

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.