
Wazanzibari kadhaa wakiongozwa
na Jumuia ya wazanzibari nchini Canada, walimu na wazee wa madrasat al-ameen na
kikundi cha darsa za wanawake cha wazanzibari cha al-hidayah, jana jumamosi
oktoba 27, 2012, walijumuika pamoja katika kuadhimisha eid al-adh-ha katika
ukumbi wa Lawrence Heights Community centre katika jimbo la north york,
Ontario.
Katika hafla hiyo, kulitolewa
mawaidha mbali mbali kama vile mmoja wa wazee wa watoto wa kizanzibari
alipowasihi wazee wenzake kuwa waumini wa kweli na kuzingatia mafundisho ya dini
yetu ya kiislamu kwa kuwafundisha watoto waishio katika nchi za kigeni maadili
ya dini yao. alisistiza kwamba kuwa na imani siyo kujiita muislamu tu bali ni
kutekeleza yake aliyotulea Allaah kupitia kwa mMume wake mpenzi Muhammad saw.
Naye Ustadhi Dullah wa Madrasat
al-Ameen aliwasihi watoto ambao walikuwapo kwa wingi katika sherehe hiyo,
kuwasikiliza wazee wao kwa kila la kheri wanalowambiwa na wache tabia ya kuguna
wanapokatazwa jambo ambalo wao wanaliona ni zuri, lakini mzee wake anafahamu
tosha kuwa halina manufaa kwao.
Alisisitiza kuwa watoto
wajishughulishe zaidi na kuwaiga wazee wao katika kutekeleza nguzo za kiislamu
kama vile kusali, kwenda misikitini siku za ijumaa wanapokuwa nyumbani, na
kufanya ibada nyengine ambazo ndizo zitakazowasaidia siku ya hesabu mbele ya
allaah. pia aliwataka wazee waache tabia ya kusema kuwa mtoto amemshinda hasiki
anayoambiwa na badala yake atumia njia za busara kumfahamisha na kumuelekeza
maadili yanayohusiana na silka za dini yetu na kizanzibari.
Naye Sheikh Abdulafatah
amewashauri wazee wazee kufanya yake yaliyoelezwa na ustadh dullah ya
kuwafundisha watoto wao yaliyo mema na kuwasisitiza kusoma qurani zaidi.
Alisema kwamba wazee watakutana
kuandaa mikakati ya kuwaelimisha watoto wetu mambo yanayohusu itikadi zetu za
kidini na kizanzibari na kuwakabidhi watoto hao wakiwa tayari kushika hatamu
hizo na baadaye waje wawachie wenzao wao watakapokuwa njia kurejea kwa Allaah.
Aliendelea kusema kuwa
mikusanyiko ya wazanzibari imepungua siku hizi kitu ambacho hakipendezi na
itakuwa vizuri kama jambo hili litaendelezwa ili wazee waweze kuwapa maarifa
watoto wao na kuwazoesha kukaa pamoja na kujuana.
Naye Ustadh Khalfan, ambaye ni
Mwalimu Mkuu wa al-ameen, alimtaka mmoja wa wanafunzi wake wahitimu, ambaye
sasa hivi ni mwanafunzi wa chuo kikuu na president wa wanafunzi wa chuo hicho,
kuwaelimisha watoto wenzake faida za elimu. Abdallah Albaalawy, aliwataka
watoto hao kujishughulisha zaidi na elimu na waache kupoteza wakati wao katika
game za computer.
Pia aliwataka watoto hao
kutokujishughulisha na masuala ya mtandao kama vile facebook na game na badala
yake waitumie computer kwa kazi zao za skuli na kujielimisha mambo ambayo hawayajui
ili kupanua akili zao. Aliwataka wafanye home work zao kwa wakati na pia
wajishughulishe na michezo zaidi kuliko kujikandamiza katika kusikiliza miziki
ya magharibi na mitandao isyowasaidia katika mustakabali wao
Hafla hiyo ilihudhuriwa na
wazanzibari kadhaa kutoka maeneo ya gta Toronto ambao kwa pamoja walifurahi
kukutana baada ya muda mrefu kutawanyika. hata hivyo, baadhi ya wazanzibari
walilazimika kuondoka kwa muda kwenda hospitali kuwawakilisha wenzao kumpa pole
mama yetu mmoja ambaye alilazwa huko na kumuombea dua ya shifaa.
Hafla hiyo ilianza kwenye milango
ya saa tisa jioni na kumalizika mnamo saa moja za jioni.
No comments:
Post a Comment