Habari za Punde

Innaa Lillaahi Wainnaa Ilayhi Raaji'uun

Mkurugenzi wa PBZ kitengo cha huduma za Benki ya Kiislam (Islamic Banking Division) , Salum Mbwana  hatunaye tena amepata ajali ya gari hivi jioni (magharibi) na kufariki papo hapo.
 
Maiti imepelekwa hospitali ya rufaa Mnazimmoja na inatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kesho asubuhi tukijaaliwa
 
Maziko saa kumi alaasiri maiti ataondokea meli nne mashine ya maji na kuzikwa kwerekwe nyoote mnaarifiwa msiba huu.
 
Marehemu huyu kwa miaka mingi pia aliwahi kuitumikia BOT , hata aliwahi kuikodi Mv. Maendeleo wakati serikali ilipoamua huibinafsisha, na kwasasa alikua ni mkurugenzi PBZ kwa uteuzi wa Rais Shein. Mungu ailaze roho yake mahali pema aamin

3 comments:

  1. Maziko saa kumi alaasiri maiti ataondokea meli nne mashine ya maji na kuzikwa kwerekwe nyoote mnaarifiwa msiba huu, marehemu huyu kwa miaka mingi pia aliwahi kuitumikia NBC bank, hata aliwahi kuikodi Mv. Maendeleo wakati serikali ilipoamua huibinafsisha, na kwasasa alikua ni mkurugenzi PBZ kwa uteuzi wa Rais Shein.

    Mungu ailaze roho yake mahali pema aamin

    ReplyDelete
  2. Shukran Mdau kwa maelezo ya ziada tumeyaambatanisha kwenye habari yenyewe

    ReplyDelete
  3. Sio NBC ni BOT amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 15 amehamia PBZ mwezi April 2012

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.