Habari za Punde

Timu Kazi ya CCM Kumsaidia Mwenyekiti wa Taifa CCM Dk. Kikwete.

 Mhe.Abdulrahaman. Kinana - Katibu Mkuu.
 Mhe. Mwigulu Nchemba - Naibu Katibu Mkuu Bara.
 Mhe. Vuai Ali Vuai - Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
 Mhe. Nape Nnauye -Katibu Mwenezi
 Mhe. Asha-Rose Migiro Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
 Mhe. Zakia Meghji - Fedha na Uchumi.
Mhe. Mohammed Seif Khatib -Oganizesheni.



WIMBI la Mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi limezidi kupamba moto baada ya Kikao cha Halmashuri Kuu kuamua kuwatema baadhi ya Watendaji katika nafasi za juu za Chama hicho
.
Hatua hiyo ya Chama cha Mapinduzi ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kukamilika kwa uteuzi huo uliofanywa na wajumbe wa kikao hicho.

Akitangaza matokeo hayo Dk Kikwete, alisema nafasi ya Katibu Mkuu CCM Tanzania, hivi sasa itakuwa inashikwa na Abrahamani Kinana, badala aya Wilson Mukama.

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Dk. Kikwete, alisema kikao hicho kimemchagua Mjumbe wa Kamati Kuu, Mwigulu Lameck Nchemba badala ya John Chiligati.

Aidha, nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, itaendelea kushikwa na Vuai Ali Vuai huku nafasi ya Katibu wa Organaizesheni itashikwa na Moahammed Seif Khatib, badala ya Asha Abdalla Juma ambapo hapo awali aliomba nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake na kushindwa kuchukua nafasi hiyo.

Nafasi ya Uchumi na Fedha, Dk Kikwete, alisema itaendelea kushikwa na Mjumbe wa NEC, Zakia Hamdan Mehgi na Nafasi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, itashikwa na Asha Rose Migiro badala Januari Makamba.

Mwenyekiti huyo alisema nafasi ya Katibu Mwenezi wa CCM itaendelea kushikwa na Nape Mnawiye, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Willson Mukama anahamishiwa nafasi ya mpya ya Mkuu wa Chuo Cha CCM na Vyama vya Ukombozi.

Nafasi za Wajumbe wa Kamati Kuu, Dk .Kikwete alisema uteuzi wake utafanyika hapo baadae kutokana na hivi sasa wajumbe hao kutingwa na shughuli nyengine.

Nafasi aliyopewa Mukama hapo awali wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa Chama hicho walipendekeza kuanzishwa kwa Chuo cha Chama ili kuweza kuwajenga wanachama wa CCM kuwa na uzalendo.

Kutokana na Mapendekezo hayo Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Kikwete, alitangaza adhma Chama hicho kuikubali dhana hiyo na kuahidi itaanzisha chuo hicho haraka iwezekanavyo.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.