Siku -
Ijumaa na Jumamosi
Tarehe –
09- 10 Muharram 1434 (23-24 November 2012)
Unachotakiwa –
Kufunga siku hizi mbili funga ya Taasu’a na ‘Aashuuraa (tarehe 9-10 Muharram)
Kwa
nini ufunge? – Kwasababu Mtume Muhammad Swalla Allaahu
‘Alayhi Wasallam alifunga na alituamrisha waislamu tufunge.
Kwa
nini Taasu’a na ‘Aashuraa? – Kwasababu Mtume Swalla Allaahu
‘Alayhi Wasallam amesema kama “Nikijaaliwa kuwa hai mwakani nitafunga na Taasua
ili kutofautiana na Mayahudi” (Muslim). Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam hakuwahi
kufika mwaka uliofuatia.
Kwa
tukio gani? Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam
alipohamia Madina aliwaona Mayahudi waliokuwa wakiishi Madina (wakati huo)
wakifunga siku hii na akauliza kwanini? Akaambiwa hii ni siku muhimu kwetu, ni
siku adhimu siku ambayo Allaah Subhaanahu Wata’ala alimwokoa Nabii Musa
‘Alayhis Salaam kutoka mikono ya Firaun. Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam
akasema, “Sisi tuna haki zaidi juu ya Musa
kuliko nyinyi” Akafunga na akaamrisha watu wafunge. ( Bukhaari)
Nini
tutarajie? Kusamehewa Madhambi yetu (madogo madogo) ya mwaka
mzima uliopita. ( Muslim)
Tumia fursa hii adhimu na
adimu kujikurubisha kwa Allaah Subhaanahu Wata’ala kwa kufunga na kuomba
Maghfira na pia kumfuata Mtume wetu na kipenzi chetu ambaye alijihimu na
kujitahidi kufunga katika siku kuliko siku nyengine yoyote ya mwaka ( isipokuwa
siku za Ramadhaan).
Please join the rest of
Muslim Ummah by fasting these two important days in Islaam. All are welcome to
join.
Tafadhali ukikufika ujumbe
huu Mkumbushe Muislamu mwenzako.
No comments:
Post a Comment