Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, wakionesha Jarida la ‘Hazina Yetu’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, baada ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, kumkabidhi Katibu Mkuu, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, amepokea Jarida la Hazina Yetu Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 linaloandaliwa na Wizara kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kila baada ya miezi mitatu.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Jarida hilo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, Katibu Mkuu, Dkt. Mwamba, alipongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Kitengo hicho katika kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi na kwa kuandaa Jarida hilo katika viwango vya hali ya juu.
Aliahidi kuwa Wizara itaendelea kikiwezesha Kitengo hicho ili kiongeze vifaa vya kisasa vya kukusanya, kuchakata na kusambaza habari kwa wadau mbalimbali wa wizara walioko ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Jarida la “Hazina yetu”limesheheni maarifa mbalimbali kupitia makala, habari, matukio, habari picha na matangazo mbalimbali na husambazwa kwa njia ya nakala ngumu (hard copies) na nakala tete (soft copies) kupitia mitandao ya kijamii ya Wizara na wadau wengine wa habari pamoja na Tovuti ya Wizara ya Fedha www.mof.go.tz
No comments:
Post a Comment