KATIBU wa Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar Asma Jidawi katikati, akitoa maelezo juu ya njia ya kuchangia mada baada ya kuwasilishwa kwa marekebisho ya sheria namba 11 ya mwaka 1999 ya kuwalinda wanyama, mbele ya wadau wa kutetea haki za wanyama kwenye mkutano wa siku moja uliofanyika ukumbi wa Magofu Chake chake Pemba jana kulia ni mwanasheria Khamis Mwita
Na Haji Nassor, Pemba
WADAU
wa kusimamia haki za wanyama,wamependekeza kuanzishwa kwa Mahakama maalum
itakayosikiliza kesi za ukatili wa wanyama, ili kupunguza ukatili huo
uliokithiri kwa wafugaji na watumiaji wengine.
Walisema katika siku za hivi karibuni
kumejitokeza kwa kiwnago kikubwa ukatili dhidi ya wanyama na ndege, bila ya
watendaji wa ukatili huo kujali wakijua kuwa hakuna adhabu itayowakumba
Wadau hao walieleza hayo jana huko ukumbi
wa Magofu Chake chake wakati walipokuwa wakichangia marekebisho ya sheria namba
11 ya mwaka 1999 ya kuwalinda wanyama ilipowasilishwa na wanasheria kutoka Tume
ya marekebisho ya sheria kupitia Wizara ya Katiba na Sheria.
Walieleza kuwa vitendo hivyo vimekuwa
vikichangiwa na kutokuwepo kwa Mahakama maalum za kushughulikia kesi za ukatili
na udahililishaji wa wanyama, hivyo kama
Wizara husika itanzisha mahakama hiyo, vitendo hivyo vinaweza kupungua kwa
kasi.
Mgeni Said Mgeni kutoka kituo cha Polisi
Chake chake, alisema pamoja kwamba kwa baadhi ya wakati kesi mbali mbali
hucheleweshwa kuanzia Jeshi la Polisi , Mahakamani na jamii yenyewe, lakini
kuwepo kwa Mahakama ya wanyama itasaidia.
Alifafanua kuwa wamiliki wa wanyama kama vile Punda na Ng’ombe wamekuwa mstari wa mbele
kutumikisha bila ya kiasi kwa kupakiwa mizigo mizito bila ya kupewa muda maalum
wa kupunzika.
‘’Wenye gari za Ng’ombe na Punda wamekuwa
wakiwapakia wanyama wao mizigo mingi na bakora juu, na anapita mbele ya vyombo
vya sheria, lakini sheria dhaifu na kutokuwepo kwa mahakama ya wanyama
kumechangia kuendelea’’.alifafanua.
Nae sheha wa Shehia ya Ndagoni Massoud Ali
Mohamed alisema uhaba wa madaktari wa wanyama kwa baadhi ya wakati, huchangia
kuingizwa kwa wanyama kutoka nje ya Kisiwa cha Pemba
bila ya kuchungzwa.
Alieleza kuwa wakati mwengine wanyama hao
wamkuwa na maradhi lakini hata wanapowakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Mapema wakiwasilisha sheria hiyo na
historia yake, mwanasheria kutoka Tume ya Marekebisho ya sheria Ali Mohamed, alisema
sheria hiyo baadhi ya vifungu haviendani na wakati uliopo ikiwa ni pamoja
adhabu ndogo kwa mkatili wa wanyama.
Nae mwanasheria Khamis Mwita wakati
akiwasilisha maoni ya sheria hiyo namba 11 ya mwaka 1999 kutoka kwa wanasheria
alisema, wamebaini kuna vipengele kadhaa ambavyo havikidhi haja kwa wakati huu
‘’Kifungu cha 36 kilikuwa kinamuelekeza
sheha na afisa mifugo kumshika mtu aliefanya ukatili dhidi ya wanyama, lakini
sisi tukapendelea sheha asiwe mkamataji bali atoe taarifa kwa vyombo vya
sheria’’,alieleza Mwita.
Tume hiyo ya marakebisho ya sheri ipo
Kisiwani Pemba kukutana na wadu mbali mbali ikiwa ni pamoja wafugaji, wataalamu
wa mifugo, maofisa Wilaya wa mifugo ili kukusanya maoni ya kuifanyia
marekebisho ya sheria hiyi namba 11 ya mwaka 1999 ya kuwalinda wanyama.
Mambo ya ajabu haya...!
ReplyDeleteIkiwa mahakama za kusimamia haki za w'damu zinatushinda itakua za wanyama?
Mfano mzuri ni lile jengo la mahakama kuu pale Viga utadhani lililohamwa!..kitu cha msingi hapa ni kupitisha mswaada wa kulinda wanyama utakaosimamiwa kisheria na kitengo ndani ya mahakama zetu!
wallahi kichekesho nasema kichekesho kwa nn ? kwa sababau zanzibar hakuna justice kabisa haheshimiwi bibadamu atatendewa haki mnyama .na kiilivyo mnayama pia anatakiwa apewe haki kama kiumbe chengine asiteswe na apate mahitaji yote muhmu kwa mmiliki wake au kwa serikali . lkn kwetu hatuna hayo wanyam wanazurura ovyo na wamechoka wanajitafutia rizki wenyewe majaani huko kwa mahakama ya wanyama zanzibar hiyo itakua ni ndoto mnajidanganya wala msizungumze tena mnatia aibu bora mnyamaze tu. msizungumze vitu ambavyo mnajua kama havitakuja ku work zanzibar.
ReplyDelete