Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman,(kushoto) akiungana na Wakuu wa Vikosi wa Ulinzi katika dhifa maalum ya Chakula kwa Askari walioshiriki katika Maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar,katika Viwanja vya Makao Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar,Iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) wakisimama na Viongozi Kamisna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa (kulia) na Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman,(wa pili kushoto) wakisimama wakati wimbo wa Taifa wa Zanzibar ulipopigwa katika hafla maalum ya Chakula kwa Askari walioshiriki katika Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akichukua Chakula wakati wa dhifa maalum ya Chakula alichowaandalia Askari walioshiriki katika Maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,katika Viwanja vya Makao
Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi
Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini, akitoa shukurani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kwa Askari walioshiriki katika Maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,kwa ushiriki wao katika dhifa maalum katika Viwanja vya Makao Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na makamanda wa vikosi vya Ulinzi walioshiki katika dhifa maalum katika
Viwanja vya Makao Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar,aliyowaandalia Askari walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Viwanja vya Makao Makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar,aliyowaandalia Askari walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
hakuna utukufu wowote ule kwenye mapinduzi hayo yalitoa roho za watu wasio na hatia , na hakuna mtukufu au utukufu ila kwa mola , haya mambo ya kutumia lugha ovyo muyaangalie kabla hamjaingia makaburini walaanifu wakubwa mliojaa rushwa , hicho chakula walichoandaliwa hao polisi ni aina ya rushwa kutoka kwa wanasiasa ambao hulindwa na askari ambao kwa bahati mbaya hawajui wanawalinda nani , jukumu la polisi ni kulinda raia na usalama wa nchi na sio wanasiasa na wala rushwa
ReplyDelete