Wanafunzi wa Madrasatul Tamima Al- Taqwa wakiingia na Kinara katika viwanja vya sherehe za kuadhimisha kwa kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW, yalioadhimishwa na madrasa hiyo katika viwanja vya madrasa yao Mpendae.
Wanafunzi wa Madrasatul Tamima Al- Taqwa wakisoma Qaswaida ya kuwakaribisha wageni waliohudhuria sherehe za maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW.
Mwalimu wa Madrasatul Tamima Al Taqwa ya Mpendae akisoma risala ya walimu wa Madrasa hiyo katika sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW,yalioandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake, huadhimishwa na Waislam wote duniani.
Mwanafunzi Is-haka Mbarouk, akisoma mlango wa kwanza Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW yaliofanyika katika viwanja vya Madrasa hiyo Mpendae
Mwanafunzi Zainab Sharif akisoma kwa njia ya Syra -Maisha ya Mtume Muhammad SAW
Mwanafunzi Tauhida Kassim, akisoma mlango wa Pili, katika Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW, akisoma kwa hibu kuonesha jinsi walivyofuzu mafundisho katika madrasa hiyo.
Wanafunzi wa Madrasatul Tamima Al- Taqwa wakionesha mchezo kwa kutumia lugha ya Kiarabu katika mafundisho kwa watoto kwa wazazi wao.
Mwanafunzi Sheikha akistafsiri Aya za Quran kwa lunga ya Kingereza kuonesha umahiri wa elimu wanayoipata katika madrasa yao, wakati wa kuadhimisha Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW yalioandaliwa na Madarasa yao Mpendae Zanzibar.
Mwanafunzi Khuzaima akisoma kwa hibu mlango wa Tatu wa Barazanji.
Mwanafunzi Masoud Suleiman akisoma Mlango wa Nne wa Barazanji, akisoma kwa hibu.
Wanafunzi wa Madrasatul Tamima Al-Taqwa wakimsalima Mtume wakati wa Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad yalioandaliwa na Madarasa hiyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Iddi, na Wazazi wakisimama kiamu wakati wa maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW.katika viwanja vya Madrasatul Tamima Al- Taqwa Mpendae.
Mgeni Rasmin wa sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW yalioandaliwa na Madrasatul Tamima Al- Taqwa Mpendae.Mama Asha Balozi Seif,akitowa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Madrasa hiyo na Wazazi waliohudhuria maulid hayo katika viwanja vya madrasa Mpendae.
Mbunge wa jimbo la Mpendae Salim Turky, akitowa shukrani baada ya kumaliza kusomwa Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW, yalioandaliwa na Madrasatul Tamima Al- Taqwa katika viwanja vya Madrasa hiyo Mpendae.
Hapo anasifiwa Mtume Muhammad (SAW) halafu tunakwenda kinyume na mafundisho yake kwa nini mgeni rasmi munamwita na jina la mume wake au hivyo ndivyo uislamu ulivyoagiza? ingekuwa hivyo na wake wa Bwana Mtume (SAW) wangeitwa kwa jina na mumwewao. ZINGATIA MAFUNDISHO YA UISLAMU SIO TUFUATE MKUMBO TU.
ReplyDelete