Habari za Punde

Utiaji wa Saini Makubaliano ya Utekelezaji wa Mradi wa TASAF-Zanzibar Awamu ya Tatu.


Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk. Khalid Salum kulia na Katibu Mtendaji wa TASAF Ladislaus .J.Mwamanga, wakitiliana saini mkataba wa  makubaliano ya Utendaji wa Mradi wa TASAF Zanzibar, baada ya kumaliza Mkutano wa siku mbili wa Kujenga Uelewa wa Mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Wajumbe wa Kamati za Uongozi na Menejimenti za TASAF - Zanzibar. utiaji wa saini hiyo umefanyika katika Ukumbe wa Karume hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk. Khalid Salum kulia na Katibu Mtendaji wa TASAF Ladislaus .J.Mwamanga, wakibadilishana mikataba ya  makubaliano ya Utendaji wa Mradi wa TASAF Zanzibar, baada ya kumaliza Mkutano wa siku mbili wa Kujenga Uelewa wa Mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Wajumbe wa Kamati za Uongozi na Menejimenti za TASAF - Zanzibar. utiaji wa saini hiyo umefanyika katika Ukumbe wa Karume hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk. Khalid Salum. akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kutiliana saini Utekelezaji wa Mradi wa Tasaf kwa Awamu Tatu. baadaya kumalizika kwa Mkutano wa Watendaji wa Mradi wa Tasaf Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtandaji wa Tasaf  Ladislaus .J.Mwamanga akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na utiaji wa saini ya Makubaliani ya Utendaji wa Miradi ya Tasaf -Zanzibar, katika Awamu ya Tatu ya Mradi huo inayoyotarajiwa kuaza hivi karibuni baada ya Kizunduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete hivi karibuni.kulia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dk. Halid Salum.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.