Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume leo (Jumapili, Jan 27, 2013) jijini Dar es Salaam ambapo aliwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema (mwenye tai) akitoka nje ya jengo la ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumapili, Jan 27, 2013) ili kupiga picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba (kulia kwake). Jaji Werema alimesilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume leo.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (kushoto) akiagana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Mrisho Sarakikya mara baada ya kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Wajumbe wa Tume uliofanyika katika ofisi za Tume leo (Jumapili, Jan 27, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni naibu Katibu wa Tume Bw. Casmir Kyuki
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Abubakar Ali akiongea katika mkutano kati ya Tume na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema leo (Jumapili, Jan 27, 2013). Kushoto ni Mjumbe mwenzake Bi. Esther Mkwizu. Katika mkutano huo Jaji Werema litoa maoni kuhusu Katiba Mpya.
Mwanasheria Mkuu Mstaafu Johnson Mwanyika akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume leo (Jumapili, Jan 27, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.
Picha na Tume ya Katiba.
No comments:
Post a Comment