Habari za Punde

Uzinduzi wa Sherehe za CCM kutimia Miaka 36 Zazinduliwa Zanzibar Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Leo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar katika sherehe za Uzinduzi wa kuzaliwa kwa CCM kutimia miaka 36., akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akifungwa kiskafu na Watoto wa Chipukizi Pili Hassan na Zadia Mbarouk, baada ya kuwasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kuzindua sherehe za kuzaliwa CCM kutimia miaka 36 zilizofanyika katika viwanja hivyo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balizo Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Silima Borafia alipowasili viwanja vya CCM Ofisi Kuu Zanzibar.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar wakiimba wimbo maalum wa Kuzaliwa Chama hicho ulioimbwa katika viwanja vya Amaani siku ya kuzaliwa CCM mwaka   5-2-1977.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiimba wimbo maalum na kupeperusha bendera ya Tanu na ASP.wakati wa uzinduzi wa sherehe za kutimia miaka 36 ya CCM. zilizofanyika kitaifa katika Viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa uzinduzi wa sherehe za kusherehekea kuzaliwa kwa CCM, zilizofanyika katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,akitowa maelezo ya sherehe za Uzinduzi wa kuzaliwa kwa CCM  zilizofanyika katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Mratibu wa Kimbe la CCM kutimia miaka 36 tangu kuzaliwa akitowa maelezo ya Michuano ya kumbea Kombe hilolitakalozishirikisha timu za Mikoa sita ya Zanzibar Minne yaUnguja na Miwili ya Pemba inayotarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa Amaan.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Silima Borafa akihutubia katika mkutano huo na kutowa salamu za Mkoa wake.hayuko pichani.
Viongozi wa Chama na Wanachama wa CCM Zanzibar wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizinduwa sherhe za kusherehekea miaka 36 ya CCM.
Waheshimiwa wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akihutubia katika sherehe hizo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikabidhiwa Kombe la Michuano yakusherehekea kuzaliwa kwa CCMnakutimiamiaka 36 na Mratibu wa Michuano hiyo na Mwakilishi wa Uzini Mohammed Raza Daramsi.  
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikabidhiwa Mipira kwa ajili ya kukabidhi kwa timu za Mikoa zinazoshiriki Michuano ya Kombe la CCM kusherehekea kuzaliwa kwa CCM na kutimiamiaka 36 na Mratibu wa Michuano hiyo na Mwakilishi wa Bububu Hussein Ibrahim Makungu  BHAA.
vya michezo vilivyokabidhiwa kwa timu za Mikoa ya sita ya Zanzibar Minne ya Unguja na Miwili ya Pemba michuano hiyo inaaza kesho uwanja wa Amaan Zanzibar.












 Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Big Star akitowa burudani katika viwanja vya Afisi Kuu yaCCM. 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein. akimkabidhi Vifaa vya michezo seti ya jezi na mipira Kiongozi wa timu ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.






Shekh akisoma dua baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kusherehekea miaka 36 ya CCM, zilizofanyikakatika viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wazee wa CCM katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar baada ya kumaliza kuzinduwa sherehe hizo ambazo zitafikia kilele chake feb 5.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.