Habari za Punde

Wananchi wa Fumba watakiwa kuutunza mradi wa mji safi na salama



Waziri wa Nchi ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk, Mwinyihaji Makame amewataka wananchi wa shehia ya Fumba kuutunza mradi wa maji safi na salama ili kuweza kufaidika na mradi huo kwa maendeleo ya shehia hiyo.
 
Ameyasema hayo wakati akizindua mradi huo uliofanyika katika shehia hiyo ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya kusherehekea miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar toka kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1964.
 
Amesema kuwa kutunzwa kwa mradi huo kutapelekea kudumu kwa muda mrefu na kuepukana na usumbufu wa kukosekana kwa maji safi na salama ambapo kutawaathiri wananchi hao.
Pia amewataka wananchi hao kuchangia huduma hiyo ya maji ili kuiwezesha mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA kuweza kutoa huduma kwa ufanisi wakati wa kutokezea kwa kuharibika kwa miundombunu ya mradi huo.
 
Aidha Dk, Mwinyihaji ameishukuru Serikali ya Japani kupitia shirika lake la maendeleo la JICA kwa kuufadhili mradi huo na kuitaka seikali ya nchi hiyo kuendelea kushirikiana na serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kutekeleza miradi mengine ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Nae mkurugenzi wa mamlaka ya maji Zanzibar Dk, Mustafa Ali Garu amesema mradi wa maji wa shehia ya Fumba unkabiliwa na changa moto ya kasi ndogo ya utokaji wa maji kutokana na uhaba wa visima pamoja na watumiaji wengi wa maji hivyo ameitaka serikali kuongeza idadi ya visima ili kupunguza tatizo hilo.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, maji na nishati amesema lengo la serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuondosha tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Unguja na Pemba hivyo amewataka wananchi kushirikiana na serikali ili kuondoa tatizo hilo.

Aidha amewataka wananchi kushirikiana na mamlaka ya maji Zanzibar kwa kuwafichua mafundi wanaoungia watu maji kiholela ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza kutokana na vitendo hivyo.
Katika risala yao wananchi wa shehia hiyo nao wameishukuru serikali ya japani kwa kuufadhili mradi huo nab kuahidi klushirikiana na mamlaka zinazohusika ili kuulinda mradi huo kwa matumizi ya muda mrefu

Pia wamesemakuwa katika shehia yao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu bwa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya maandalizi jambo linalorudisha nyuma kiwango cha elimu hivyo wamitaka serikali kuwajengea madarasa hayo ili watoto waweze kusoma

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.