Na
Pascal Michael, Musoma
WATU
wawili wamekufa katika matukio mawili tafauti akiwemo mtu mmoja
anayefahamika kwa jina la
Kashimiri Suleman Ndobo (40) mkazi wa Buhare manispaa ya Musoma alikutwa
akiwa amekufa na mwili wake kutupwa katika gofu la nyumba.
Hayo yamesemwa
jana na Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Kamishina msaidizi Absalom
Mwakyoma wakati akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari.
Mwakyoma
alisema marehemu wakati wa uhai wake aliwahi kuwa Afisa
Utamaduni kabla ya kuacha kazi kutokana na maradhi ya akili yaliyosababishwa na kuchanganyikiwa.
Polisi
wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake.
Katika
tukio la pili mtu mmoja asiyejulikana jina
amekutwa amefariki dunia katika eneo la Makoko manispaa ya Musoma.
Mwakyoma
alisema mwili wa marehemu
anaekadiriwa kuwa na umri kati ya
miaka 24 -27 ulikutwa umetupwa kando ya Ziwa
Victoria.
Alisema
hadi sasa hakuna mtu aliyeutambua mwili huo na maiti imehifadhiwa katika chumba
cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
mkoa wa Mara kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari.
No comments:
Post a Comment