Na
Hassan Hamad, OMKR-Morogoro
CHAMA cha
kimesema Watanzania wanahitaji kuleta mabadiliko katika kujenga uchumi imara wa
nchi yao.
Mwenyekiti
wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba alieleza hayo wakati
akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya saba saba Morogoro mjini,
ikiwa ni mwendelezo wa operesheni mchaka mchaka iliyoanzishwa na chama hicho
kwa mikoa mbali mbali ya Tanzania.
Alisema
uchumi wa Tanzania
unaweza kuimarika iwapo serikali itaweka mipango imara ya kukuza uchumi ikiwa
ni pamoja na kutumia rasilimali za nchi kwa maslahi ya wananchi.
“Tunataka
kila Mtanzania aweze kunufaika moja kwa moja na rasilimali za nchi hii, mapato
yatokanayo na maliasili yanaweza kuwa
makubwa, kwa nini wananchi nao wasinufaike?” alihoji Prof. Lipumba.
Alisema
tatizo kubwa linaloikabili Tanzania kwa sasa ni uongozi usiokuwa na dira ya
uhakika wa mabadiliko, na kutaka Watanzania wafanye maamuzi ya kubadilisha safu
ya uongozi na kuwapa madaraka viongozi wenye dira watakaoweza kuleta mabadiliko
ya kiuchumi.
Alisema
iwapo CUF kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi mwaka 2015 kitahakikisha kuwa
kinatekeleza mipango yake ya kukuza na kuimarisha uchumi ili kunyanyua kipato
cha wananchi.
“Morogoro
kwa mfano ardhi yake inakubali kuotesha kila aina ya mazao lakini wananchi wake
bado ni maskini kutokana na kutokuwepo mipango imara ya kuimarisha na
kuendeleza kilimo,” alifafanua Prof. Lipumba.
Akizungumzia
kuhusu vitambulisho vya Taifa, Prof. Lipumba amewahimiza wananchi kujisajili
ili kupata vitambulisho hivyo wakati utakapofika.
Alisema
licha ya utambulisho wa Watanzania, lakini vitambulisho hivyo pia ni muhimu
katika mipango ya maendeleo.
Alisema
vitambulisho hivyo ambavyo vinatumia teknolojia ya kisasa na alama za mwili,
vinaweza kutumika hata katika mgao wa gawio litokanalo na mapato ya rasilimali
iwapo serikali itaamua kufanya hivyo.
Alifahamisha
kuwa miaka 51 ya uhuru bado Tanzania haijakuwa na umeme wa uhakika, hali
inayosababisha wawekezaji kushindwa kuwekeza viwanda vikubwa na kuzorotesha
maendeleo ya kiuchumi.
Nae
Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema rasilimali za nchi
bado hazijawanufaisha ipasavyo Watanzania, na badala yake zimekuwa
zikiwanufaisha zaidi wageni jambo ambalo linahitaji kuangaliwa upya.
Alisema
baadhi ya vyama vikuu vya siasa nchini tayari vimeonesha kupoteza mwelekeo, na
kuwaomba wananchi kuendelea kukiunga mkono CUF ili kiweze kuleta mabadiliko ya
kweli.
“Chama
chetu siku zote kinaendelea kuhubiri juu ya dhamira yake ya kuwaunganisha
Watanzania na kuleta mabadiliko ya kweli ya kiuchumi ili kila kila mwananchi
apate haki sawa na mwengine, sambamba na kuondosha kabisa matabaka haya ya
wananchi wa daraja la kwanza, la pili na la tatu,” alifafanua Maalim Seif.
Aliwapongeza
wananchi wa Morogoro kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo licha ya
kuibuka kwa mvua kubwa iliyosababisha mtafaruku na kuleta hofu ya kuvurugika mkutano
huo.
Alisema
mvua hiyo ambayo imekosekana kwa kipindi kirefu mkoani humo, ni dalili tosha
kuwa chama hicho ni chama cha baraka, na kuwaomba wananchi wandelee kukiunga
mkono ili kutimiza malengo yake.
Katika
hatua nyengine aliyekuwa Mwenyekiti wa vijana CHADEMA jimbo la Ukonga,
Mchungaji Calistus Titus aliweka wazi baadhi ya sababu zilizompelekea kujiengua
katika chama hicho mwezi uliopita na
kuamua kujiunga na CUF.
Mchungaji
huyo wa kanisa la Gongo la mboto “Ulongoli B”, alisema alichoshwa na tabia ya
viongozi wa chama hicho kutokana na jazba walizonazo katika kuendesha chama,
pamoja na kuwepo ufisadi wa kutisha ndani ya chama hicho.
Alisema
alivutiwa na CUF baada ya kuona kuwa viongozi wake ni watu wenye busara na
mwelekeo thabiti wa kuleta ukombozi wa kweli kwa Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment