Na Mwajuma Juma,DSM
MWENYEKITI
wa chama cha ADC Taifa, Said Miraji amesema kukosekana uzalendo wa viongozi
kumepelekea nchi kuporomoka.
Akizungumza
na wanachama na viongozi wa chama hicho katika hoteli ya Cresto Palace iliyopo
Bungoni Dar es Salaam,alisema hao yote yametokana na kukosekana kwa miiko na
maadili ndani ya vyama.
Alisema
uzalendo umepungua sana kiasi kwamba inafikia
pahala watu kusahau miiko na maadili yao
na kupelekea kugombana.
Miraji
alisema kumekuwa na mambo mengi
yanafanyika
kinyume na matakwa ya wananchi ikiwemo kujengwa barabara zilizo chini ya
kiwango na mambo mengine ya maendeleo ambayo mara
nyingi
hutokea vitendo vya wizi, rushwa, na wananchi kuchukuwa sheria mikononi mwao.
“Mzalendo
maisha yote hahitaji kusukumwa katika kufanya jambo ambalo litakuwa na maslahi
ya taifa,” alisema.
Hata
hivyo alisema, iwapo uzalendo utarejeshwa kutaondoa nusu ya matatizo yaliyomo
katika nchi yao, hivyo aliwataka viongozi wa chama hicho kuwa wazalendo ili
kuwa mabalozi wazuri katika ushindani wa kimaendeleo.
Kuhusu
mchakato wa katiba mpya, Miraji alisema kuandikwa kwa katiba hiyo bila ya
kuigusa katiba ya Zanzibar
ni sawa na kupiga pasi suruali mguu mmoja.
Alisema
kama kweli kunafanyika marekebisho ya katiba hayo hakunabudi na katiba ya Zanzibar ikaandikwa upya
hasa kwa vile katiba
iliyopo
sio wanayoitaka wananchi wa Zanzibar.
Alisema
pamoja na hayo pia katiba hiyo inahitaji kuandikwa upya ili kuepusha
maingiliano ya vifungu vya sheria pamoja na kutokea suintafahamu kutokana na
kifungu kimoja kukataza na chengine kukubalia
jambo.
No comments:
Post a Comment