JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
MWONGOZO KUHUSU MUUNDO, UTARATIBU
WA KUWAPATA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA YA
WILAYA (MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA) NA UENDESHAJI WAKE
1.0. UTANGULIZI
Kwa mujibu wa Kifungu cha 18 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, Tume inawajibu wa kuunda Mabaraza
ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba
iliyoandaliwa na Tume. Muundo wa Mabaraza ya Katiba unapaswa kuzingatia mgawanyiko
wa kijiografia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Mabaraza ya Katiba yatawashirikisha
na kuwakutanisha wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii
kwa lengo la kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba. Aidha, kifungu cha 17 (8)
kinaeleza kuwa, isipokuwa kama mazingira yatahitaji
vinginevyo, Tume itabuni utaratibu unaofanana ambao utatumika kila upande wa
Muungano.
Kifungu cha 18 (6) kinaeleza aina nyingine ya Mabaraza ya
Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu kidogo cha (6), Tume inaweza kuruhusu Asasi,
Taasisi au Makundi ya watu kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa
wanachama wake kutoa maoni yao
juu ya Rasimu ya Katiba na kisha kuwasilisha maoni hayo kwa Tume.
Ili kuendana na muda wa kuwapata Wajumbe na kufanyika kwa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa pamoja na maandalizi
yote muhimu, vikao vya kupendekeza majina na kufanya uchaguzi vitafanyika kwa
utaratibu ufuatao:-
Kwa Msingi huo,
Tume imeamua kuwa Mabaraza ya Katiba yatakuwa katika makundi mawili yafuatayo:-
1.1
Mabaraza ambayo Tume itayasimamia na kukusanya Maoni
(Mabaraza ya Katiba ya Wilaya – Ngazi ya
Mamlaka ya Serikali za Mitaa).
1.2
Mabaraza ambayo Tume haitayasimamia. Mabaraza hayo
yatajisimamia yenyewe na kukusanya maoni yatakayowasilishwa kwenye Tume kwa
mujibu wa maelekezo. (Mabaraza ya Katiba
ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu).
Mwongozo huu unaainisha Muundo, Utaratibu wa kuwapata Wajumbe na Utaratibu wa Uendeshaji
wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
yatakayoendeshwa na kusimamiwa na Tume.
2.0. MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA NGAZI YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Kwa kuzingatia mgawanyiko wa kijiografia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya – Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa yataundwa
kwenye kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika ngazi ya Halmashauri za Jiji,
Manispaa, Mji, Wilaya na Mabaraza ya Miji.
Kwa upande wa Tanzania Bara, Katika Mikoa yote ngazi ya kupata wajumbe wa
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya (Mamlaka za Serikali za Mitaa) itakuwa ni Ngazi ya
Kata. Wajumbe watapigiwa kura za kupendekezwa kwenye ngazi za Kijiji/Mitaa na
kuchaguliwa kwenye ngazi ya Kata.
Kwa upande wa Zanzibar, Katika Mikoa yote ngazi ya kupata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya
Wilaya (Mamlaka za Serikali za Mitaa) itakuwa ni Shehia. Wajumbe watapigiwa kura
kwenye ngazi za Shehia.
Muundo na utaratibu huu umezingatia changamoto mbalimbali
zikiwemo; ukubwa wa Mabaraza ya Katiba, utaratibu wa kuwapata wajumbe, ufanisi
katika uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba, gharama ya kufanikisha shughuli ya
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, na tofauti
ya Mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar .
Kutokana na changamoto hizo, utaratibu wa kuwapata
wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya haufanani kwa pande zote za Muungano.
3.0.
WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA NGAZI YA
MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
3.1
Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba.
Mabaraza ya Katiba katika ngazi ya Halmashauri za
Jiji, Manispaa, Mji, Wilaya na Mabaraza ya Miji yataundwa na Wajumbe wafuatao:-
3.1.1. Kwa Tanzania
Bara.
3.1.1.1
Wajumbe wanne
kutoka kila Kata watachaguliwa kwautaratibu utakaofafanuliwa na Mwongozo huu.
3.1.1.2
Wajumbe wanane
kutoka kila Kata kwa Mkoa wa Dar es Salaam .
3.1.2. Kwa Zanzibar .
3.1.2.1.
Wajumbe watatu
kutoka kila Shehia watachaguliwa kwa utaratibu utakaofafanuliwa na Mwongozo
huu.
3.1.3. Kwa pande
zote za Muungano.
3.1.3.1.
Madiwani
wa kuchaguliwa kwenye Kata / Wadi.
3.1.3.2.
Madiwani
wa Viti Maalum.
3.1.3.3.
Madiwani
wa kuteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa pande zote za
Muungano [Madiwani waliopo kazini kwa sasa].
3.2
Ngazi ya Msingi ya kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba
3.2.1. Kwa upande
wa Tanzania
Bara
Kwa Mikoa
yote ya Tanzania Bara, ngazi ya msingi ya kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba itakuwa Kata.
3.2.2. Kwa upande
wa Zanzibar
Kwa Mikoa
yote ya Zanzibar ,
ngazi ya msingi ya kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba itakuwa Shehia.
3.3
Idadi ya Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya
ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Idadi
ya Wajumbe itakuwa kama ifuatavyo:-
3.3.1. Kwa
Tanzania Bara, idadi ya Mabaraza ya
Katiba yatakayoendeshwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni 163 ambapo kila Mamlaka moja ya
Serikali za Mitaa ngazi ya Wilaya itakuwa na Baraza moja la Katiba ukiondoa
Mkoa wa Dar es Salaam
ambapo kila Halmashauri itakuwa na Mabaraza mawili ya Katiba. Hivyo, jumla ya
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa itakuwa 163 (zipo Mamlaka za Serikali za Mitaa 160).
3.3.2. Katika Mikoa 24
ya Tanzania Bara, kila kata itawakilishwa na Wajumbe wanne (4) ambao wataungana na Madiwani wa Kata
na Viti Maalum. Idadi ya Kata ni 3,339 ukiondoa
kata 90 za Mkoa wa Dar
es Salaam , zinabaki kata 3,249
[utaratibu wa kuwapata wajumbe kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni tofauti na Mikoa mingine ya
Tanzania Bara na umefafanuliwa katika aya ya 3.3.3]. Hivyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kutoka kwenye Kata
zote isipokuwa kata 90 za Mkoa wa Dar
es Salaam , watakuwa 12,996 na idadi ya Madiwani wote ni 4,453.
3.3.3. Kwa Mkoa wa Dar
es Salaam , wenye Kata 90 utawakilishwa na Wajumbe wanane (8) kutoka kila Kata. Kwa hiyo, idadi ya Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya kutoka Mkoa Dar es Salaam Watakuwa
720 watakaoungana na Wajumbe wengine
kama ilivyofafanuliwa kwenye aya ya 3.3.2.
Jumla
ya Wajumbe wote wa Mabaraza ya Katiba kwa Tanzania Bara watakuwa 18,169 kwa mchanganuo ufuatao:-
3.3.3.1.
Idadi ya
Wajumbe 4 kutoka kila Kata 12,996
3.3.3.2.
Idadi ya
Wajumbe 8 kutoka Kata za Mkoa wa
Dar es salaam 720
3.3.3.3.
Idadi ya
Madiwani wote ni: 4,453
18,169
|
JUMLA:
3.3.4. Kwa upande
wa Zanzibar, idadi ya Mabaraza ya
Katiba yatakayoendeshwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni 13 ambapo kila Mamlaka moja ya Serikali
za Mitaa itakuwa na Baraza moja la Katiba (zipo
Mamlaka za Serikali za Mitaa 13).
3.3.5. Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 13 za Zanzibar , kila Shehia
itawakilishwa na Wajumbe watatu (3)
ambao wataungana na Madiwani wa Wadi, Viti Maalum, na Wakuteuliwa waliopo
kazini kwa sasa. Idadi ya Shehia ni 335.
Hivyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kutoka kwenye Shehia zote
watakuwa 1,005 na idadi ya Madiwani
wote ni 193.
Jumla
ya Wajumbe wote wa Mabaraza ya Katiba kwa Zanzibar
watakuwa 1,198 kwa mchanganuo
ufuatao:-
3.3.5.1.Idadi ya Wajumbe kutoka kila Shehia:
1,005
3.3.5.2.Idadi ya Madiwani Wote ni: 193
1,198
|
JUMLA
Mchanganuo
wa idadi ya Wajumbe kwa kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kama ilivyo kwenye Jedwali
“1” kwa upande wa Tanzania Bara na Jedwali
“2” kwa Zanzibar.
4.0.
SIFA ZA WATAKAOCHAGULIWA KUWA WAJUMBE WA MABARAZA
YA KATIBA YA WILAYA NGAZI YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA
MITAA.
Wajumbe
wanne kutoka kila Kata kwa Tanzania Bara na wanane kutoka kila Kata katika Mkoa
wa Dar es Salaam na Wajumbe watatu kutoka kila Shehia
kwa Zanzibar wanapaswa
kuwa na sifa zifuatazo kwa pamoja:-
4.1
Awe ni Raia
wa Tanzania .
4.2
Awe na
umri wa miaka 18 au zaidi.
4.3
Awe na
uwezo wa kusoma na kuandika.
4.4
Awe ni mkazi
wa kudumu wa Kijiji/ Mtaa / Shehia husika.
4.5
Awe ni Mtu
mwenye hekima, busara na uadilifu.
4.6
Awe ni Mtu
mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo.
5.0.
MAMBO YA KUZINGATIWA
Licha
ya sifa zilizotajwa katika aya ya 4.0.,
utaratibu wa kuwapata Wajumbe kwa Tanzania Bara na Zanzibar uzingatie mambo yafuatayo:-
5.1
Uwakilishi wa watu wazima.
5.2
Uwakilishi wa wanawake.
5.3
Uwakilishi wa vijana, yaani kati ya miaka 18 hadi 35.
5.4
Jiografia ya Kata/ Wadi / Kijiji / Mtaa / Shehia husika.
6.0.
UTARATIBU WA KUWAPATA WAJUMBE KWENYE MABARAZA YA
KATIBA YA WILAYA NGAZI YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
6.1
Kwa upande wa Tanzania
Bara utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-
Kwa Mikoa
yote isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam .
6.1.1. Kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, kila Mwananchi wa Kijiji / Mtaa husika anayependa kuwa Mjumbe
wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa atawasilisha
jina lake kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa.
Uwasilishaji huo uambatane na taarifa zifuatazo:-
6.1.1.1.
Majina
kamili ya mwombaji.
6.1.1.2.
Jinsi
yake.
6.1.1.3.
Umri wake.
6.1.1.4.
Elimu
yake.
6.1.1.5.
Kazi yake.
6.1.1.6.
Sehemu
anayoishi katika Kijiji / Mtaa husika.
6.1.2. Wakati wa uwasilishaji wa jina, kila mwananchi
anayependa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya, atawasilisha nakala mbili
za barua kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa. Nakala moja ibaki kwa Afisa
Mtendaji wa Kijiji / Mtaa; na nakala ya pili iwekwe Mhuri na saini ya Afisa
Mtendaji wa Kijiji / Mtaa. Nakala hiyo abaki nayo mwanachi husika kwa
uthibitisho kuwa barua yake ilipokelewa.
6.1.3. Orodha ya majina ya Wananchi wote wanaotaka kuwa Wajumbe
yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi / matangazo ya kila Ofisi za Kijiji / Mtaa
siku saba (7) kabla ya Mkutano ili wananchi wapate fursa ya kuyapitia na
kujiridhisha kama walioomba wana sifa
zilizoanishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0.
6.1.4. Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa ataitisha Mkutano
Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa ambao utakuwa na agenda moja tu ya kuwapendekeza
kwa kuwapigia kura watu wanne ambao majina yao yatawasilishwa kwenye Kamati ya Maendeleo
ya Kata. Mkutano huu utaendeshwa na Mwenyekiti wa Kijiji / Mtaa, ambapo Afisa Mtendaji
wa Kijiji / Mtaa atakuwa Katibu wa Mkutano huo na ndiye atakayewasilisha majina
ya wananchi wote walioomba kuingia kwenye Baraza la Katiba la Wilaya.
6.1.5. Kwa kuzingatia Sifa zilizoainishwa katika aya za 4.0. na 5.0, Mkutano Mkuu Maalum wa
Kijiji / Mtaa utayapigia kura ya siri majina ya wananchi walioomba kuwa Wajumbe
wa Baraza la Katiba la Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
6.1.6. Utaratibu wa kupiga kura za kwenye Mkutano Mkuu
Maalum wa kuwachagua Wananchi wanne wanaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya utakuwa kama ifuatavyo:-
6.1.6.1.
Kwanza , Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya
siri ya kumchagua Mtu mzima mmoja [anaweza
kuwa mwanamke au mwanamme].
6.1.6.2.
Pili,
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya siri ya kumchagua
Mwanamke mmoja.
6.1.6.3.
Tatu,
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya siri ya
kumchagua Kijana mmoja [anaweza kuwa
Mwanamme au Mwanamke].
6.1.6.4.
Nne,
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya siri ya kumchagua Mtu mwingine yeyote kutoka miongoni
mwa Wananchi walioomba kuwa Wajumbe wa Baraza la katiba la wilaya.
6.1.7. Orodha ya majina ya wananchi wanne waliopigiwa
kura nyingi za kupendekezwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ngazi ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa, yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi/ matangazo ya
kila Ofisi ya Serikali ya Kijiji / Mtaa.
6.1.8. Majina ya watu wanne yatakayokuwa yamepata kura
nyingi kuliko mengine yatawasilishwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa kwa
Afisa Mtendaji wa Kata yakiwa yameambatanishwa na Muhtasari wa Mkutano Mkuu Maalum
wa Kijiji / Mtaa uliosainiwa na Mwenyekiti wa Kijiji /Mtaa pamoja na orodha ya
wananchi waliohudhuria.
6.1.9. Afisa Mtendaji wa Kata baada ya kupokea majina
yaliyopendekezwa kutoka kwenye Mikutano Mikuu Maalum ya Vijiji / Mitaa ya Kata
husika, ataitisha Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, ambacho kwa
kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0 kitachagua
majina manne kwa kura ya siri kwa utaratibu ufuatao:-
6.1.9.1.
Kwanza , Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri ya
kumchagua Mtu mzima mmoja [anaweza
kuwa mwanamke au Mwanamme].
6.1.9.2.
Pili,
Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri ya kumchagua Mwanamke mmoja.
6.1.9.3.
Tatu,
Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri ya kumchagua Kijana mmoja [anaweza kuwa Mwanamme au Mwanamke].
6.1.9.4.
Nne,
Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri ya kumchagua Mtu
mwingine yeyote kutoka miongoni mwa
wananchi walioomba kuwa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya.
6.1.10. Jina la Mwananchi atakayekuwa amepata kura nyingi
kutoka kila kundi [Mtu mzima, Mwanamke,
Kijana na Mtu mwingine yeyote] yatawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Serikali za Mitaa yakiwa na Muhtasari uliosainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa
Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata kilichoyapigia kura majina hayo
pamoja na orodha ya Wajumbe waliohudhuria.
6.1.11. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia
sifa na utaratibu ulioainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, atawasilisha
majina kwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa Uteuzi.
6.1.12. Endapo Diwani wa kata ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati ya Maendeleo ya Kata hatakuwepo [Kwa sababu zozote ikiwa ni pamoja na
kuwa safarini kwa kipindi ambacho Mabaraza ya Katiba yatafanyika, kuwa mgonjwa
na kutoweza kutekeleza majukumu ya Udiwani, Kifo au sababu nyingine], utaratibu
wa kawaida wa kumpata mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata
wakati Diwani hayupo utatumika, ambapo Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa
atakayependekezwa na Wajumbe wenzake wa Kamati ya Maendeleo ya Kata kuendesha
Kikao hicho ndiye atawakilisha kata badala ya Diwani.
6.2
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam
utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-
6.2.1. Kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, kila Mwananchi wa Mtaa husika anayependa kuwa Mjumbe wa
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa atawasilisha
jina lake kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa. Uwasilishaji
huo uambatane na taarifa zifuatazo:-
6.2.1.1.
Majina
kamili ya mwombaji.
6.2.1.2.
Jinsi
yake.
6.2.1.3.
Umri wake.
6.2.1.4.
Elimu
yake.
6.2.1.5.
Kazi yake.
6.2.1.6.
Sehemu
anayoishi katika Mtaa husika.
6.2.2. Wakati wa uwasilishaji wa jina, kila mwananchi
anayependa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya, atawasilisha nakala mbili
za barua kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa. Nakala moja ibaki kwa Afisa Mtendaji wa
Mtaa; na nakala ya pili iwekwe Mhuri na saini ya Afisa Mtendaji wa Mtaa. Nakala
hiyo abaki nayo mwanachi husika kwa uthibitisho kuwa barua yake ilipokelewa.
6.2.3. Orodha ya majina ya Wananchi wote wanaotaka kuwa
wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa,
itawekwa kwenye maeneo ya wazi / matangazo ya Ofisi za Mtaa kwa siku saba (7)
kabla ya Mkutano ili wananchi wa Mtaa husika wapate fursa ya kuyapitia na
kujiridhisha kama walioomba wana sifa zilizoanishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0.
6.2.4. Afisa Mtendaji wa Mtaa ataitisha Mkutano Mkuu Maalum
wa Mtaa ambao utakuwa na agenda moja tu kuwapendekeza kwa kuwapigia kura ya
siri watu Wanane watakaokuwa wajumbe wa Mabaraza ya katiba ya Wilaya ngazi ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa.
6.2.5. Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa wa kuwachagua wananchi
wanane (8) kuwa Wajumbe wa Mabaraza
ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa utaendeshwa na
Mwenyekiti wa Mtaa ambapo Afisa Mtendaji wa Mtaa atakuwa Katibu, na ndiye
atakayewasilisha majina ya wananchi wote kwenye Mkutano huo walioomba kuingia
kwenye Baraza la Katiba la Wilaya.
6.2.6. Utaratibu wa kupiga kura za kwenye Mkutano Mkuu Maalum
wa Mtaa wa kuwachagua Wananchi wanane wanaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza
ya Katiba ya Wilaya utakuwa kama ifuatavyo:-
6.2.6.1.
Kwanza , Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura ya siri ya kuwachagua Watu
Wazima Wawili [wanaweza kuwa Wanawake au Wanaume].
6.2.6.2.
Pili,
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura ya siri ya kuwachagua
Wanawake wawili.
6.2.6.3.
Tatu,
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura ya siri ya kuwachagua
Vijana wawili [wanaweza kuwa Wanaume
au Wanawake].
6.2.6.4.
Nne,
Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura za siri kuwachagua Watu
wengine wawili wowote kutoka miongoni mwa majina yaliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa
Mtaa.
6.2.7. Orodha ya majina ya Wananchi wanane waliopigiwa
kura nyingi za kupendekezwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ngazi ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa, yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi/ matangazo ya
kila Ofisi ya Serikali ya Mtaa.
6.2.8. Majina ya watu wanane yatakayokuwa yamepata kura
nyingi kuliko mengine, yatawasilishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa kwa Afisa
Mtendaji wa Kata yakiwa yameambatanishwa na Muhtasari wa Mkutano Mkuu Maalum wa
Mtaa uliosainiwa na Mwenyekiti wa Mtaa pamoja na orodha ya Wananchi
waliohudhuria.
6.2.9. Afisa Mtendaji wa Kata baada ya kupokea majina
yaliyopendekezwa kutoka kwenye Mikutano Mikuu Maalum ya Mitaa ya Kata husika,
ataitisha Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, ambacho kwa kuzingatia
sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na
5.0 kitachagua majina manane kwa
kura ya siri kwa utaratibu ufuatao:-
6.2.9.1.
Kwanza , Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri ya
kuwachagua Watu wazima wawili [wanaweza
kuwa Wanawake au Wanaume].
6.2.9.2.
Pili,
Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kuwachagua Wanawake wawili.
6.2.9.3.
Tatu,
Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kuwachagua Vijana wawili [wanaweza kuwa wanaume au
wanawake].
6.2.9.4.
Nne,
Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kuwachagua watu wawili wengine wowote, kutoka
miongoni mwa majina yaliyowasilishwa kwenye Kikao Maalum cha Kamati ya
Maendeleo ya Kata.
6.2.10.
Majina ya
Wananchi watakaokuwa wamepata kura nyingi kutoka kila kundi [Watu wazima wawili, Wanawake wawili, Vijana
wawili na Watu wawili wengine] yatawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Serikali za Mitaa yakiwa na Muhtasari uliosainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa
Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, kilichoyapigia kura majina hayo
pamoja na orodha ya Wajumbe waliohudhuria.
6.2.11. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa
kuzingatia sifa na utaratibu ulioainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, atawasilisha
majina kwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa Uteuzi.
6.2.12. Endapo Diwani wa Kata ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati ya Maendeleo ya Kata hatakuwepo [Kwa sababu zozote ikiwa ni pamoja na
kuwa safarini kwa kipindi ambacho Mabaraza ya Katiba yatafanyika, kuwa mgonjwa
na kutoweza kutekeleza majukumu ya Udiwani, kifo au sababu nyingine], utaratibu
wa kawaida wa kumpata Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata
wakati Diwani hayupo utatumika, ambapo Mwenyekiti wa Mtaa atakayependekezwa na
Wajumbe wenzake wa Kamati ya Maendeleo ya Kata kuendesha Kikao hicho ndiye
atawakilisha kata badala ya Diwani.
6.3
Kwa upande wa Zanzibar utaratibu utakuwa kama
ifuatavyo:-
6.3.1. Kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, kila Mwananchi Mkaazi wa Shehia husika anayependa kuwa mjumbe
wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa
atawasilisha jina lake
kwa Sheha. Uwasilishaji huo
uambatane na taarifa zifuatazo:-
6.3.1.1.
Majina
kamili ya mwombaji.
6.3.1.2.
Jinsi
yake.
6.3.1.3.
Umri wake.
6.3.1.4.
Elimu
yake.
6.3.1.5.
Kazi yake.
6.3.1.6.
Sehemu
anayoishi katika Shehia husika.
6.3.2. Wakati wa uwasilishaji wa jina, kila Mwananchi
anayependa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya, atawasilisha nakala mbili
za barua kwa Sheha. Nakala moja ibaki kwa Sheha; na nakala ya pili iwekwe Mhuri
na saini ya Sheha. Nakala hiyo abaki nayo Mwanachi husika kwa uthibitisho kuwa
barua yake ilipokelewa.
6.3.3. Orodha ya majina ya Wananchi wote walioomba kuwa Wajumbe
wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi (mfano Skuli) / matangazo katika Shehia
husika siku saba (7) kabla ya Mkutano ili Wananchi wapate fursa ya kuyapitia na
kujiridhisha kama walioomba wana sifa zilizoanishwa
kwenye aya za 4.0 na 5.0.
6.3.4. Sheha ataitisha Mkutano wa Shehia husika ambao
utakuwa na agenda moja tu ya kuwapigia kura ya siri watu watatu [3] ambao
majina yao
yatawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Katibu wa Halmashauri Mji/
Wilaya ambapo Shehia hiyo ipo.
6.3.5. Mkutano wa Shehia utachagua Mwenyekiti na Katibu
wa Mkutano huo kutoka miongoni mwa Wananchi waliohudhuria Mkutano. Katibu ndiye
atakayewasilisha kwenye Mkutano majina
ya Wananchi wote walioomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi
ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
6.3.6. Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano wa Shehia
watakaochaguliwa sharti wawe na sifa kama za Wajumbe
wa Mabaraza ya Katiba zilivyoainishwa katika aya ya 4.0.
6.3.7. Utaratibu wa kupiga kura kwenye Mkutano wa Shehia
wa kuwachagua Wananchi watatu kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya
utakuwa kama ifuatavyo:-
6.3.7.1.
Kwanza , Wananchi wote waliohudhuria Mkutano wa Shehia watapiga kura ya siri
ya kumchagua Mtu mzima mmoja [anaweza
kuwa Mwanamke au Mwanamme].
6.3.7.2.
Pili,
Wananchi wote waliohudhuria Mkutano wa Shehia watapiga kura ya siri ya
kumchagua Mwanamke mmoja.
6.3.7.3.
Tatu,
Wananchi wote waliohudhuria Mkutano wa Shehia watapiga kura ya siri ya kumchagua
Kijana mmoja [anaweza kuwa Mwanamme
au Mwanamke].
6.3.8. Matokeo ya upigaji kura wa siri yatatangazwa kwenye
Mkutano baada ya mchakato wa kupiga kura kukamilika na kuwekwa kwenye maeneo ya
wazi / matangazo katika Shehia husika.
6.3.9. Katibu wa Mkutano wa Shehia, atawasilisha majina
ya watu watatu (3) waliochaguliwa katika
Mikutano ya Shehia kwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Katibu wa Halmashauri
ya Mji / Wilaya ambapo Shehia hiyo ipo katika muda wa siku moja tangu Mkutano
ulipofanyika. Mawasilisho hayo yaambatane na muhtasari wa Mkutano uliotiwa
saini na Mwenyekiti na Katibu pamoja na orodha ya majina ya wananchi
waliohudhuria.
6.3.10. Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Katibu wa
Halmashauri Mji/ Wilaya kwa kuzingatia sifa na utaratibu ulioainishwa kwenye
aya za 4.0 na 5.0, atawasilisha majina kwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
kwa uteuzi.
Baada ya kupokea orodha ya majina ya watu
waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ,
Katibu atatoa barua rasmi za kuwateua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya
ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
7.0.
TARATIBU ZA KUFANYA MIKUTANO YA KUWAPATA WAJUMBE
WA MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA.
7.1
Wananchi
wanaopenda kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wawasilishe majina yao kwa Maafisa Watendaji wa Vijiji / Mitaa kwa Tanzania
Bara na kwa Sheha kwa Zanzibar
kati ya tarehe 08 Machi, 2013 hadi 20 Machi,
2013.
7.2
Orodha ya
majina ya Wananchi wote wanaotaka kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa iwekwe
kwenye maeneo ya wazi / matangazo katika Ofisi za Vijiji / Mitaa kwa Tanzania
Bara; na katika maeneo ya wazi / matangazo kwenye Shehia husika kwa Zanzibar tarehe 22 Machi, 2013 na majina hayo
yaendelee kuwepo hadi tarehe 28 Machi, 2013.
7.3
Kwa Tanzania Bara, Vikao vya Vijiji / Mitaa vya kuwachagua kwa
kuwapigia kura za siri wananchi wanne kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba vifanyike
kati ya tarehe 30 Machi 2013 hadi 03
Aprili, 2013.
7.4
Kwa upande wa Tanzania Bara, Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata cha
kuwachagua wajumbe wanne kutoka miongoni mwa Wananchi waliopigiwa kura na Mikutano
Mikuu ya Vijiji / Mitaa kifanyike kati ya tarehe
05 Aprili 2013 hadi 09 Aprili, 2013.
7.5
Kwa Tanzania Bara, majina ya Wajumbe wanne waliochaguliwa na Kikao Maalum cha Kamati ya
Maendeleo ya Kata, yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa
husika kati ya tarehe 13 Aprili, 2013 hadi
17 Aprili, 2013.
7.6
Kwa Mkoa wa Dar
es Salaam ,
7.6.1. Vikao vya Mitaa vya kuwapigia kura ya
kuwapendekeza wajumbe wanane wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya vifanyike kati ya tarehe 30 Machi, 2013 hadi 03 Aprili, 2013.
7.6.2. Vikao Maalum vya Kamati za Maendeleo za Kata vya
kuwachagua wajumbe wanane kutoka miongoni mwa wananchi waliopigiwa kura na
Mikutano Mikuu ya Mitaa vifanyike kati ya
tarehe 05 Aprili, 2013 hadi 09 Aprili, 2013.
7.6.3. Majina ya Wajumbe wanane waliochaguliwa na Kikao
Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Serikali za Mitaa husika kati ya
tarehe 13 Aprili 2013 hadi 17 Aprili,
2013.
7.7
Kwa Zanzibar ,
7.7.1.
Vikao vya Shehia vya kuwachagua kwa
kuwapigia kura za siri Wananchi watatu kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya vifanyike kati ya tarehe 30 Machi, 2013 hadi 03 Aprili, 2013.
7.7.2.
Majina ya Wajumbe watatu, waliochaguliwa
na Mikutano ya Shehia, yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa,
Katibu wa Halmashauri ya Mji / Wilaya ambapo Shehia hiyo ipo kati ya tarehe 13 Aprili 2013 hadi 17 Aprili, 2013.
Majina
ya watu wote waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,
pamoja na majina ya Madiwani wote wa Mamlaka ya Serikali za Mtaa husika yawasilishwe
kwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kutumia Fomu maalum iliyoandaliwa
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa madhumuni hayo kwa njia ya nakala tete (soft
Copy) na nakala mango (hard copy) kati ya tarehe 25 Aprili 2013 hadi 30 Aprili, 2013.
8.0.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MCHAKATO WA KUWAPATA
WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA
Ni
Jukumu la Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia, kuratibu na
kuhakikisha Mikutano hiyo inafanyika.
8.1
Kwa Tanzania Bara isipokuwa kwa Mkoa wa Dar es
Salaam
8.1.1.Mikutano yote ya Vijiji / Mitaa itaendeshwa na
Wenyeviti wa Serikali za Vijiji / Mitaa na Maafisa Watendaji wa Vijiji / Mitaa
watakuwa ni Makatibu na wasimamizi wa Mikutano hiyo.
8.1.2.Mikutano Mikuu yote ya Vijiji / Mitaa itakayoitishwa
kwa lengo la kuwapigia kura ya siri watu wanne kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya vifanyike katika tarehe moja kwenye Vijiji / Mitaa yote
iliyopo kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika.
8.1.3.Vikao vyote vya Kamati za Maendeleo za Kata
vitakavyokuwa na jukumu la kuwachagua watu wanne kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa vifanyike katika tarehe
moja kwenye Kata zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika.
8.1.4. Kwa Mkoa
wa Dar es Salaam :
8.1.4.1.
Mikutano
Mikuu yote ya Mitaa itakayoitishwa kwa lengo la kuwapigia kura watu wanane
wanaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ifanyike katika
tarehe moja kwenye Mitaa yote iliyopo kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa
husika.
8.1.4.2.
Vikao vyote vya Kamati za Maendeleo za Kata
vitakavyokuwa na jukumu la kuwachagua watu wanane kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa vifanyike katika tarehe
moja kwenye Kata zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika.
8.2
Kwa Zanzibar
8.2.1. Ni jukumu la Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa,
Katibu wa Halmashauri ya Mji / Wilaya kusimamia,
kuratibu na kuhakikisha Mikutano hiyo inafanyika.
8.2.2. Mikutano yote ya Shehia itaendeshwa na Wenyeviti
na Makatibu watakaochaguliwa na Mikutano hiyo.
8.2.3. Jukumu la Sheha ni:-
8.2.3.1.
Kupokea
majina ya Wananchi wanaoomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
8.2.3.2.
Kubandika katika maeneo ya wazi /
matangazo majina yote ya watu walioomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya
Wilaya.
8.2.3.3.
Kuitisha
Mkutano wa Shehia utakaochagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano.
8.2.4. Majukumu ya Katibu wa Mkutano atakayechaguliwa:-
8.2.4.1.
Kupokea
orodha ya majina ya Wananchi wote walioomba
kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kutoka kwa Sheha.
8.2.4.2.
Kuwasilisha
majina ya Wananchi wote walioomba
kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwenye Mkutano.
8.2.4.3.
Kuratibu
mchakato wa uchaguzi kwenye Mkutano.
8.2.4.4.
Kubandika
kwenye maeneo ya wazi / matangazo matokeo ya kura kwa kila mwombaji alivyopata
baada ya Mkutano.
8.2.4.5.
Kuandaa
Muhtasari wa Mkutano.
8.2.4.6.
Kuwasilisha
majina ya Wananchi walioshinda pamoja na Muhtasari wa Mkutano kwa Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo kwenye Shehia husika.
9.0.
MABARAZA
YA KATIBA YA ASASI, TAASISI NA MAKUNDI YA WATU
Kama
ilivyoelezwa hapo awali, Kifungu cha 18 (6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
Sura ya 83, kinaeleza aina nyingine ya Mabaraza ya Katiba. Tume inaruhusu Asasi, Taasisi au Makundi ya
Watu wenye malengo yanayofanana kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa
wanachama wake kutoa maoni yao
juu ya Rasimu ya Katiba kisha kuwasilisha maoni hayo kwa Tume si zaidi ya tarehe 14 Agosti, 2013.
Mabaraza hayo yatajiendesha yenyewe na kuwasilisha
maoni yao kwa
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Orodha ya Mabaraza hayo ni pamoja na:
1.1.
Jumuiya ya
kidini.
1.2.
Chama cha
siasa.
1.3.
Asasi ya
kiraia.
1.4.
Taasisi ya
elimu ya juu.
1.5.
Chama cha
wafanyakazi.
1.6.
Chama cha
wakulima.
1.7.
Chama cha
wafugaji.
1.8.
Chama cha
Wanahabari.
1.9.
Mabaraza
ya Watoto, Taasisi za Kitaaluma, Vijana na Wazee.
1.10.
Kundi au
makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kama
Sheria inavyoelekeza.
1.11.
Kundi au makundi ya watu wenye mahitaji maalum
katika jamii.
10.0.
TAREHE YA KUANZA KUTUMIKA
Mwongozo
huu utaanza kutumika kuanzia tarehe 01
Machi, 2013.
Joseph S. Warioba
Mwenyekiti
Tume ya Mabadiliko ya Katiba
No comments:
Post a Comment