Habari za Punde

Wazanzibar Wanaoishi Canada watowa Vifaa kwa Walemavu Zanzibar

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Fatma Ferej, akitowa shukrani kwa Wazanzibar wanaoishi Nchini Canada kwa msaafa wao kwa watoto wenye ulemavyu, Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Wazanzibar Wanaoishi Canada (ZanCan ) makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Welemavu Welesi Zanzibar leo.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al Masroori akizungumza na Wazazi wa watoto wenye ulemavu hawapo pichani katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao,kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji huko  Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles.
 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akiwa na Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada Bishara Al Masroori wakimkadhi baskeli ya walemavu Mtumwa Hamadi Khamis mkaazi wa Tomondo huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada  (ZANCANA) Bishara Al Masroori akiwa na Mtoto mlemavu Amur Yunus Hamadi aliyebebwa na Baba ake akiwa na Toizi ya kuchezea huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.