Habari za Punde

DKT. Bilal Afungua Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka wa Wadau wa PSPF.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Jubilee Towers, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka, wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika. katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kitambulisho, Faridi Ibrahim Kiringi, mfanyabiashara wa duka la Nguo, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Hati na Nyumba na funguo, Adorat Francis Milinga, mmoja kati ya watu watano walionunua nyumba za PSPF, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa
 Msanii, Mrisho Mpoto,(Mjomba) akitoa burudani mbele ya jukwaa kuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na watumishi wa mfuko huo, baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa pili wa mwaka wa Wadau wa PSPF, leo.Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.