Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.
PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Machi
31, 2013 ametembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili kuwapa pole majeruhi walioumia katika ghorofa
lililoporomoka juzi Ijumaa Machi 26, 2013 katika Mtaa wa Indira Ghandi jijini
Dar es salaam na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 20.
Rais
Kikwete, akiwa ameongozana na mke wake, Mama Salma Kikwete, pamoja na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa
Ghasia, aliwatembelea na kuwapa pole majeruhi Mohamed Ally Dhamji, Baqir Virani,
Selemani Saidi na Yusuf Abdallah waliolazwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
Majeruhi
hao, ambao kwa mujibu wa Daktari C.N. Mcharo wanaendelea vyema na matibabu na
hali zao ni za kuridhisha, ni wanne ni kati ya sita waliolazwa katika taasisi
hiyo, ambapo wawili wamekwisharuhusiwa.
"Poleni sana kwa maumivu mliyoyapata na
nawatakia mpate nafuu ya haraka", Rais Kikwete aliwaeleza majeruhi
hao, walionusurika baada ya kuangukiwa na jengo hilo la ghorofa 16
lililoporomoka ghafla likiwa katika ujenzi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31
Machi, 2013
No comments:
Post a Comment