Habari za Punde

Nahodha ahutubia wanachama wa CCM Mzalendo, Magomeni

 Mjumbe wa Kamati kuu CCM na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha akikabidhi kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama cha Mapinduzi huko katika mkutano wa Hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Uwanja wa Mzalendo Magomeni Mjini Zanzibar.
 Wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wakiwa wamehudhuria katika Mkutano wa hadhara wa chama hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mjumbe wa Kamati kuu CCM na Muakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe aidha pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha hapo Magomeni katika kiwanja cha Mzalendo Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh akisalimiana na wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na kueleza mambo mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo hilo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Uwanja wa Mzalendo Magomeni Mjini Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati kuu CCM na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Uwanja wa Mzalendo Magomeni Mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

2 comments:

  1. hicho kiriri aliposimama Shamsi Nahodha kuhutubia kinachefua, basi angalau wangekipamba kwa kanga kikapendeza. Haya basi kitieni rangi kipendeze kama mlivyopendeza wenyewe na sare zenu.

    ReplyDelete
  2. Yaani..Shamsi ni bonge moja la kiongozi! na kama sio ile 'attitude' ya shemegi zangu kwamba nusu ya viongozi wote wa SMZ lazma watoke 'KAE'

    ningesema akiwa president zanzibar lazma itabadilika!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.