Habari za Punde

Waziri wa Uvuvi Azinduwa Uwekaji Matumbawe ya Bandia Baharini.

Waziri wa Uvuvi  na Mifugo Abdilah Jihad, akizungumza na Viongozi wa Uvuvi na Maofisa wa KMKM , kuhusiana na kutunza Matumbawe ya baharini  ambayo ni mazalio ya samaki na kuna baadhi ya wavuvi huaribu kwa makusudi kutumia uvuvi haramu ya baruti na bunduki.
Wafanyakazi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar  wakitayarisha Matumbawe ya Bandia kwa kutumia mapira ya gari ili kuyaweka baharini kuwa mazalio ya samaki.wakiwa katika pwani ya Marubi .
Mfanyakazi wa Idara ya Uvuvi akiyatosa matumbawe bandia baharini ili kuwa ni mazalio ya samaki kutokana na baadhi ya wavuvi  kuyaharibu matumbawe kwa uvuvi haramu.
 Mfanyakazi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Kapteni Haji Shomari akizamia kuweka matumbawe bandia katika bahari ya marumbi Unguja.
  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.