Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja alipoanza ziara ya kuangalia
maendeleo ya Mkoa huo jana,huko Tunguu Wilaya ya Kati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim,akitoa ufafanuzi kuhusu kuhusu masuala ya Kilimo ,uwezeshaji wananchi kiuchumi,wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,iliyoanzia jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tunguu na kutembelea Vijiji Mbali mbali kuangalia maendeleo ya Kijamii katika Wilaya ya Kati
Mkurugenzi Mkuu wa Malaka ya Maji ZAWA Dk.Mustafa Ali Garu,wa pili kushoto)akitoa maelerzo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa tangi la Maji safi,ambapo ujenzi wake unajengwa na
kampuni kutoka China,akiwa katika ziara ya Wilaya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa Machui Wilaya ya Kati Unguja,baada ya kuangalia maendeleo ya hatua za mwanzo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa tangi la maji safi,akiwa katika ziara ya Mkoa wa \Kusini Unguja jana,(kulia)Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati,Ramadhan Abdalla Shaaban
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo alipofuatana na Mkurugenzi wa Ujenzi Idara ya Ujenzi Ramadhan Mussa Bakari,(wa tatu kulia) wakati alipotembelea ujenzi wa Nyumba ya Serikali ya Mpapa ambayo iko katika hatua za mwisho wa ujenzi,alipokuwa katika ziara ya Wilaya ya kati Unguja jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akimuuliza suala Mkurugenzi wa Ujenzi Idara ya Ujenzi Ramadhan Mussa Bakari,(wa tatu
kulia) wakati alipotembelea ujenzi wa Nyumba ya Serikali ya Mpapa ambayo iko katika hatua za mwisho wa ujenzi,alipokuwa katika ziara ya Wilaya ya kati Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea vifaa vya miundombinu ya Maji safi vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, wakati alipotembelea ujenzi wa Nyumba ya Serikali ya Mpapa ambayo iko katika hatua za mwisho wa ujenzi,alipokuwa katika ziara ya Wilaya ya kati Unguja jana.(Picha Ramadhan Othman -Ikulu)
No comments:
Post a Comment