Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi alipofanya ziara ya Mkoa huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea Ripoti ya utendaji kazi za Mkoa,kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,alipofika Ofisini kwake akiwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza leo
Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Idara mbali mbali za Ofisi za Serikali wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,katika mkutano na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akionesha zawadi aliyopewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,(katikati) alipofika Ofisini kwake akiwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza leo,(kushoto) Mkuu wa Wilaya Mjini Abdi Mahmoud Mzee
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mhandisi wa Ujenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Iddi Khatib,alipotembelea kukagua Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya huko Mpendae Mjini Zanzibar,akiwa katika
Pichani Ujenzi Skuli ya Sekondari ya Wilaya huko Mpendae Mjini Zanzibar ukiendelea katika Mkoa wa Mjini Magharibi ,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alitembelea ujenzi huo akiwa katika ziara ya Mkoa huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo ya Ujenzi kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Iddi Khatib,alipotembelea kukagua Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya huko Mpendae Mjini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji (ZAWA) DK.Mustafa Ali Garu,alipofika Chumbuni Kuangalia mradi uchimbaji wa kisima cha Maji katika eneo hilo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Hassan Ali Mbarouk,(kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Hassan Ali Mbarouk,(wa pili kushoto) wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
No comments:
Post a Comment