Habari za Punde

Dk Shein akutana na uongozi wa Wizara ya elimu na mafunzo ya amali

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana asubuhi,( kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad

Baadhi ya Watendaji na maafisa wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,katika kikao cha utekelezaji wa Kazi za Wizara hiyo, kilichofanyika jana chini mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
 
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Na Rajab Mkasaba , Ikulu

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar inatarajia kutoa mikopo kwa wanafunzi wapya 1600 kwa mwaka 2013/2014 ili kukabiliana na ongezeko la idadi kubwa ya wanafunzi wanaopata sifa za kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Hayo yameelezwa jana katika kikao cha uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, Ikulu Zanzibar wakati Wizara hiyo ikieleza utekelezaji wa mpagokazi wake kwa kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013.
Akitoa maelezo ya utangulizi wa mpango kazi huo, Waziri wa wizara hiyo Mhe, Ali Juma Shamuhuna alisema kuwa hatua hiyo inatokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaopata sifa za kuendelea na masomo ya elimu ya juu ambao huhitaji kikopo kutoka Bodi ya ikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar.
Uongozi wa Wizara hiyo ulieleza changamoto iliyopo hivi sasa kwa baadhi ya wadaiwa wa mikopo hiyo mara baada ya kuanza zoezi la kutakiwa kurejesha fedha walizokopa baada ya kumaliza masomo yao kuwa wagumu kurejesha ambapo Wizara ilisisitiza mashirikiano kwa wale wote waliokopa fedha hizo ili na wengine waweze kufaidika.
Aidha, Wizara hiyo ilieleza kuwa kati ya skuli 19 mpya za Sekondarei zinazojengwa kupitia mkopo wa Benki ya Dunia, skuli 13, zimekamilika na zote hivi sasa zinatumika ambapo kati ya hizo tano ziko Unguja na nane ziko Pemba.
Uogozi wa Wizara hiyo ulieleza kuwa kukamilikamkwa skuli hizo kumesaidia sana Wizara katika kuongeza nafasi za kusoma kwa wanafunzi wa Sekondarina kupunguza msongamano wa wanafunzi katika baadhi ya skuli.
Pia, uongozi huo ulieleza kuwa ujenzi wa skuli ya msingi ya Mwanakwerekwe inayojengwa kwa msaada wa Serikali ya China umekamilika na skuli itakabidhiwa kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika mwezi huu wa Aprili 2013.
Waziri alisema kuwa ukarabati wa skuli ya Sekondari Utaani na Fidel Castro kwa Pemba na Tumekuja kwa Unguja umekamilika na skuli hizo hivi sasa zinatumika ambapo kwaupande wa ukarabati wa Skuli ya Uweleni, Pemba na Forodhani pamoja na Hamamni Unguja unaendelea vizuri na skuli hizo zinatarajiwa kukamilka mwanzoni mwezi ujao.
Katika kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa, Wizara hiyo ilieleza kuwa kwa kuazia bajeti ya mwaka 2013/2014, inakusudia kutoa kipaumabele katika kukamilisha ujenzi wa madarasa 500 yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo idadi hiyo itasaidia kuongeza nafasi na kupunguza msongamano wa wanafunzi katika madarasa.
Wizara ilielezamkuwa inakususdiaa kuanzisha utaratibu wa kuzizawadia skuli zinazofaya vizuri sana kwa kutoa zawadi zenye thamani kubwa kwa skuli inayofaya vizuri, zaidi ya utaratibu uliyopo sasa wa kumzawadia mwanafunzi mmoja mmoja.
Aidha, Wizara iliahidi kuendelea kuwapatia walimu mikopo ya kununua vipando na vifaa vya ujenzi kwa ajiliya kuwasaidia kuikamkazini kwa wakati hasa walimu wanaosemesha maeneo ya mbali.
Sambamba na hayo, Wizara hiyo ilieleza azma yake ya kuanzisha Skuli ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Chuo Kikuu cha Cuba ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa madaktari hapa nchini.
Nae Rais Dk. Shein kwa upande wake alitoa pongezi kwa uongozi na watendaji wa Wizara hiyo kwa juhudi wanazozichukua katika kuendeleza sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kusifu mpangilio mzuri wa Mpango kazi wa Wizara hiyo ulivyowasilishwa.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja kwa wakuu wa Wizara na Idara zote za Wizara hiyo na pamoja na Wizara nyenginezo za Serikali ya ,Mapinduzi Zanzibar kuwa na utamaduni wa kuzungumza na wafanyakazi wao ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Alieleza kuwa ni jambo la busara kiongozi kuzungumza na wafanyakazi wake na ndipo kazi zitakapofanyika kwa ufanisi na ubora zaidi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein pia, alieleza umuhimu kwa uongozi wa Wizara kutoa taarifa katika vyombo vya habari hasa ikizingatiwa kuwa Wizara hiyo imefanya mambo mengi ya msingi tokea kwa Mapinduzi matukufu ya Januari 12,1964 ambapo hapo mwakani yanatimiza miaka 50.
“Sisi serikalini tumeamua kuzungumza na waandishi wa habari katika ila baada ya mda tuliopaga, hivyo na nyinyi itumieni nafsi hii kwa kueleza mafanikio yenu kwani mnayo mengi”,alisisitiza Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuimarishwa kwa ukaguzi maskulini ili kukuza kiwango cha elimu nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.