Na Asya Hassan
WAHANDISI 23 kutoka India watakaokifanyia matengenezo kiwanda cha sukari Mahonda wamewasili nchini tayari kuanza kazi hiyo, kabla ya uzalishaji bidhaa hiyo kuanza mwishoni mwa mwaka huu.
Jopo la wahandisi hao linaongozwa na Mshauri Mkuu wa kilimo cha sukari, Ummashan Kar Misra.
Mshauri elekezi wa kiwanda, hicho Dk. Hamza Hussein Sabri alieleza hayo alipozungumza na gazeti hili.
Alisema kufika kwa wataalamu hao kutakuwa chachu ya kuweza kufanikisha ukarabati wa kiwanda hicho na kuweza kufanya kazi zake kama kawaida.
Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza kazi za kuzalisha sukari wakati wowote baada ya kukamilika ukarabati na matengenezo ya mashine.
Kiongozi wa wahandisi hao, Ummashan Kar Misra alisema lengo la kuja Zanzibar ni kukarabati kiwanda na mashine za kutengenezea sukari pamoja na kutoa ujuzi kwa wananchi wa Zanzibar juu ya uzalishaji sukari ili kuweza kujitegemea wenyewe.
No comments:
Post a Comment