Habari za Punde

CUF yatangaza mgombea Chambani


Khamis Haji, OMKR
 
CHAMA cha CUF kimemtaja mwanachama wake, Yussuf Salim Hussein kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Chambani katika uchaguzi mdogo uliopangwa kufanyika Juni 16 mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Uenezi wa CUF, Salum Abdalla Bimani, jina la mgombea huyo limepitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho katika kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichoanza juzi.
 
Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilijadili majina ya wagombea 12 waliojitokeza kuwania kuteuliwa na chama kuwania nafasi ya hiyo.
 
Nafasi ya ubunge Jimbo la Chambani iko wazi kufuatia kufariki dunia kwa aliyekuwa Mbunge wake kupitia chama cha CUF, marehemu Salim Hemed Khamis, Machi 20, mwaka huu.
 
 
Kampeni za uchaguzi huo zimepangwa kuanza Mei 18.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.