Habari za Punde

Jumuiya za CCM zampongeza Dk. Shein


Na Khamisuu Abdallah
 
JUMUIYA za chama cha Mapinduzi (CCM) zimempongeza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuvuna idadi kubwa ya wanachama katika ziara zake za kichama Unguja na Pemba.

Jumuiya hizo zimesema sasa zinaamini safari ya ushindi wa CCM unaendelea kwa kasi kubwa na kwamba jumuiya hizo zimejipanga kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola.

Akizungumza kwa niaba ya Jumuiya za UVCCM, UWT na Wazazi, Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Salama Aboud Talib alisema kumalizika kwa ziara hiyo kumewafanya wanachama na wapenzi wa CCM kuwa na imani na chama chao.


Aidha alisema Dk. Shein alikuwa na moyo wa ujasiri na kuonesha utayari wa kukitumikia chama kwa kuwa anapenda watu na umoja ili kuleta maendeleo nchini.

"Sisi Jumuiya tatu za CCM tunajua wazi kuwa ziara hii ya Makamu Mwenyekiti imeongeza nguvu na ufanisi katika kutekeleza majukumu yetu ya kukisafisha njia chama chetu na kuhakikisha kinapata ushindi milele," alisema.

Hivyo aliwasihi wananchi kuendeleza amani na utulivu na kutii amri ya viongozi wao.

Katika ziara hizo, Dk. Shein alivuna wanachama 5,448, kati yao 139 wanatoka vyama vya upinzani.

1 comment:

  1. acha wewee ,subirini mtapoingia makaburini mwenu ndio mtajua kama mmevuna au mmevunwa.
    ccm chama cha majambazi
    ccm chama cha mabepari
    ccm chama cha makabaila
    ccm chama cha madhalimu
    ccm chama cha mtanganyika
    ccm chama cha maadui , nafikiri hazimaliziki hizi ...

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.