Habari za Punde

Mnara wa Weles.

Mabaki ya Mnara wa Kihistoria wa Mawasiliano Weles Kikwajuni  Zanzibar.
 
 Enzi hizo uliokuwa ukipokea Mawasiliano kutoka Nchini Aden, Yemen na kusambazwa katika sehemu za Afrika Mashariki, na kwa hivi karibuni ulikuwa ukitumiwa na Kampuni za Simu za Mkononi kwa kuweka mitambo yao.
 
Umefunguliwa kwa ajili ya kuwekwa kituo cha Mawasiliano ya Mkonge wa Taifa. Sehemu hiyo itatumika kwa ajili ya matumizi ya Kupokelewa Mawasiliano na kurusha sehemu husika katika Visiwa vya Zanzibar.    
 
Niliwahi kusimuliwa kwamba kulikuwa na shetani hapa alikuwa na mguu mmoja tena wa kike. Kama ni kweli sijui atakuwa amehamia wapi kama bado yupo.

5 comments:

  1. yupo kitoto chake kina mkono mmoja maskani yake jamhuri garden..juu ya mpera

    ReplyDelete
  2. Yupo ubavani mwa spitali ya mnazimmoja na anajicho moja

    ReplyDelete
  3. Hiyo Ndio Faida ya Mapinduzi Gharamu yaliofanywa 1964.. Ati Muafrica alikua hana hakki.. Uzandiki Mtupu wa Watwana Walioingia Zanzibar kutafuta kazi baadae wakajifanya wanauchungu wa Visiwa hivi nakuua Maelfu ya Wazanzibari.

    SMZ tokea ilipochukua Nchi inajua kutumia tu lakini hakuna kinachotengenezwa... Majumba ya Mjini yamejaa kutu na Unguku. Halafu utasikia kuna Baraza la Mji.

    ReplyDelete
  4. Wacha kuchanganya mambo, kama unataka kuikosa SMZ kosoa tu, ni haki yako ya kikatiba na kimsingi wameshindwa kuvisimamia visiwa hivi ipasavyo.

    Lakini kuhusu mapinduzi lazma ukubali ukweli "ukataka, usitake yameshafanyika aliyekufa kafa na aliyepona kapona ukweli utabaki huo"

    Hapa hakuna cha mtwana wala muungwana nchi ni yetu sote na itabaki kua hivyo!

    Uzembe upo na mimi nakuunga mkono kwa hilo lakini na sisi ni sehemu ya uzembe huo kwani sisi ndio tuliowachagua!

    ReplyDelete
  5. Tatizo la watu wengi wa Zanzibar ni kujikomba kuwa Waarabu wakati historia iko wazi. Hao tunaowaita watwana na wajakazi kutoka bara ndio wazazi wetu. Hata hao waliopakapaka rangi basi wazee wao wa upande wa kike ni wanyamwezi, wamanyema, wasukuma, wamakonde n.k waarabu hawakuja na wanawake hapa zanzibar. Wao wanaojiita bahasani, baalawi, lemky, miskri wote wanadamu za kinyamwezi, au kisukuma au kimakonde. Sasa ya nini katika karne hii bado wewe kijana una mawazo ya utwana na ujakazi? Hebu muulize bibi yako au babu yako anatoka wapi? Unazungumza uzembe wakati mkikutana kwenye baraza la wawakilishi mazungumzo yenu muungano tuuu basi. Sasa huo uzembe umeletwa na muungano? Acheni unafiki?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.