Habari za Punde

Nyuki, JKU wanawake wang’ara kikapu

 
Na Mwajuma Juma

TIMU ya mpira wa kikapu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Zanzibar) Nyuki,imeendeleza ubabe mbele ya warembo wa African Magic baada ya kuirusha roho kwa vikapu 40-30 katika ligi kanda ya Unguja uliochezwa uwanja wa Maisara.

Timu hizo zote zilishuka uwanjani zikiwa na pointi
mbili kila moja, baada ya kushinda katika michezo yao ya awali.
 
Katika mchezo uliofuata, kinadada wajenga uchumi wa JKU, wakawafundisha New West kwa kuwamiminia vikapu 52-33.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo miwili kwa timu za wanawake, ambapo wakati wa saa 9:00 mchana, JKU itatiana mikononi na Nyuki, huku African Magic na New West wakipapatuana mnamo saa 10:00 jioni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.