Habari za Punde

Ataka kujua utaratibu wa fedha za jimbo Zanzibar

Na Mwandishi wetu , Dodoma
 
MBUNGE wa Viti Maalumu Tauhida Cassian Gallos (CCM) ameihoji serikali kuhusu utaratibu wa fedha za maendeleo ya majimbo zinazopelekwa Zanzibar.
 
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Salum Hassan, alisema kila mwaka wa fedha, Ofisi ya Makamu wa Rais hupokea fedha za maendeleo ya majimbo kutoka Wizara ya Fedha ya Muungano.
 
“Fedha hizo hupokelewa  kwa ajili ya majimbo ya Zanzibar yaliyopo,” alisema Hassan.
 
Alisema baada ya kupokea fedha hizo, Ofisi ya Makamu wa Rais huzipeleka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo huziwasilisha Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
 
Alisema ofisi hiyo baada ya kuzipokea huzisambaza fedha hizo kwa halmashauri za wilaya ili zigawanywe kwa majimbo husika.
 
Chanzo - Tanzania Daima

1 comment:

  1. Haya ndio mambo W'bari tunayotakiwa kujua na sio ushabik usio na msingi.

    Mimi binafsi sielewi kazi za halmashauri za wilaya Z'bar, hebu anaejua anieleweshe.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.